Mkurugenzi wa M-Pesa, Bw. Epimack Mbeteni (katikati) akiwa amejumuika na wateja kupata huduma za M-Pesa kwenye banda la Vodacom Tanzania katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyoanza Juni 28 hadi Julai 13, 2023 katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika msimu huu wa Sabasaba watanzania watarudishiwa mpaka 10% ya pesa wakilipia bidhaa kwa simu (M-Pesa). Vile vile wanayo fursa ya kununua simu kwa bei nafuu kwa pesa taslimu au mkopo na kunufaika na hadi GB 96 kwa mwaka. Huduma nyingine ni pamoja na kuunganishwa Vodabima na kupata router za intaneti za 5G. |
No comments:
Post a Comment