Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Tuesday, 18 July 2023
NBC YAWAPA FURSA WAKAZI WA MWANZA KULISHUHUDIA KOMBE LA LIGI KUU YA NBC
Wadhamini wakuu wa ligi ya Tanzania bara maarufu kama Ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), imewapelekea wakazi wa jiji la Mwanza kombe jipya la ubingwa wa ligi hiyo namba tano kwa ubora barani Afrika.
Kwa mujibu wa NBC, lengo la kulipeleka kombe hilo mkoani Mwanza, ni kuwapa fursa wateja wa benki hiyo, wapenzi wa soka na wakazi wa jiji hilo kwa ujumla, fursa ya kulishuhudia na kupiga nalo picha kombe hilo jipya.
Shughuli ya kulishuhudia kombe, imeenda sambamba na fursa ya kupata huduma mbali mbali za kibenki kwa wakazi wa jiji hilo kutoka katika benki hiyo kongwe na yenye mtandao mpana wa matawi hapa nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment