Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 23 June 2023

HUDUMA YA NBC CONNECT YAGONGA HODI MKOANI DODOMA

Meneja wa NBC tawi la Dodoma Japhet Fungo akiuelezea Mfumo wa NBC Connect namna unavyoweza kurahisisha ufanyaji wa miamala kidigitali kwa wateja wa benki hiyo katika Hafla ya Uzinduzi wa mfumo huo iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ally Gugu (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa meneja wa benki ya NBC tawi la Dodoma Japhet Fungo muda mfupi baada ya uzinduzi wa huduma ya NBC Connect katika Hafla ya Uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya NBC Connect inayowezesha kufanya miamala kwa urahisi kwa njia ya kidigitali. Hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo ilifanyika jijini Dodoma.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa huduma ya NBC Connect, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ally Gugu (watatu kulia)akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya NBC na baadhi ya wateja walioalikwa kwenye uzinduzi wa huduma ya NBC Connect inayowezesha kufanya miamala kwa urahisi kwa njia ya kidigitali. Hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.

Dodoma Juni 21, 2023: Makampuni pamoja na taasisi mbali mbali ambazo ni wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara ya (NBC) mkoani Dodoma, sasa wanaweza kupata uzoefu mpya wa huduma za kibenki kupitia huduma ya kibenki kwa njia ya kidigitali inayojulikana kama ‘NBC Connect’

NBC Connect, ni huduma ya kisasa ya kidigitali kwa makampuni na taasisi mbali mbali, ambayo huwezesha huduma salama za kibenki kufanyika sehemu yoyote, muda wowote kwa njia ya mtandao.

Huduma hii ni sehemu ya mchango wa benki katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuongeza ujumuifu katika huduma za kifedha (financial inclusion) kwa makundi mbali mbali.

Uzinduzi wa huduma ya NBC Connect Dodoma, ni wa tatu baada ya uzinduzi uliofanyika kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya na wa Kanda ya ziwa uliofanyika Mwanza.

Kupitia NBC Connect, wateja wenye makampuni na taasisi zilizopo mkoani Dodoma na maeneo ya jirani, wataweza kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi zaidi na kupata uzoefu mpya.

Huduma itawapa wateja uwezo wa kufanya miamala kirahisi ikiwa ni pamoja na malipo ya ndani na nje ya nchi, malipo ya Serikali pamoja na malipo kwa mkupuo bila kuchukua muda kwa kutumia simu au kompyuta. Wateja pia wataweza kupata taarifa za miamala waliyofanya popote pale walipo pasipo kulazimika kwenda benki.

NBC Connect imebuniwa kwa teknalojia ya kisasa na yenye usalama wa hali ya juu ambayo imezingatia na kutoa kipaumbele kwenye usiri wa taarifa za mteja. Ubunifu wa huduma hiyo huakikisha taarifa za kifedha za wateja zinalindwa wakati wote.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa NBC tawi la Dodoma Japhet Fungo alisema, "Tunafuraha kutambulisha NBC Connect kwa wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani. Mfumo huu wa kibenki wa kidigitali ni uthibitisho wa dhamira ya kuwapatia wateja wetu huduma bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama, na kukidhi mahitaji ya yao. NBC Connect itawawezesha wateja wetu wenye makampuni na taasisi mbali mbali kufanya huduma za kibenki popote pale, wakati wowote, na kufurahia huduma hizo bila matatizo."

Pamoja na huduma rahisi na za kisasa, NBC Connect itatoa usaidizi binafsi kwa wateja kupitia kituo chake cha huduma kwa wateja ambapo mameneja wetu wanapatikana ili kuwasaidia wateja kulingana na mahitaji yao nakutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia huduma hilo kwa ufanisi.

"Tunawaalika wateja wetu wote wa Dodoma na maeneo ya jirani wajionee urahisi na usalama wa NBC Connect. Ni huduma ambayo inaleta mapinduzi mapya kwenye namna ambavyo huduma za kibenki zinatolewa. Tuna uhakika kuwa wateja wetu watafaidika nayo kwa kiasi kikubwa , "aliongeza

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Katibu Tawala wa Mko wa Dodonma Ally Gugu aliishukuru Benki ya NBC kwa ubunifu wao mzuri na kuwahimiza wateja kutumia mfumo huo mpya wa kibenki ili kurahisisha shughuli zao za kibenki.

“Uzinduzi wa NBC Connect Dodoma unawakilisha mpango mkakati wa upanuzi wa benki ya NBC ili kufikia taasisi mbali mbali na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Benki ya NBC inasifika kwa dhamira yake ya kuwajibika kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii kupitia mipango mbalimbali, kama vile Mbio za Kimataifa za NBC Dodoma Marathon zinazohamasisha matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, msaada wa afya ya uzazi kupitia kliniki zinazotembea, programu za elimu ya kifedha, uwezeshaji wa vijana. kupitia udhamini wa Ligi Kuu ya NBC, hakika napongeza juhudi hizi zinazofanywa na NBC” alisema

Kuhusu Benki ya NBC:

Benki ya NBC ni taasisi ya kifedha inayoongoza nchini Tanzania inayotoa bidhaa na huduma mbalimbali za kibenki kwa watu binafsi, wafanyabiashara na jamii. Kwa kujitolea kwa dhati kwenye suala la huduma kwa wateja, uvumbuzi, na uwajibikaji wa kijamii, NBC Connect inalenga kuwa mshirika wa benki anayeaminika kwa watu binafsi na biashara Tanzania nzima.

No comments:

Post a Comment