Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Thursday, 16 March 2023

WASHINDI 7 WAPATIKANA DROO YA TATU YA BIA YA PILSNER 'KAPU LA WANA'

Afisa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries, Emila Tom Machuve (kulia) akizungumza na mmoja wa washindi wa promosheni ya bia ya Pilsner ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ wakati wa droo ya tatu ya promosheni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania, Salim Mgufi akisimamia mchakato huo. Kwenye droo hiyo, walipatikana washindi saba kutoka kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini ambapo promosheni ya Kapu la Wana inafanyika.

Kati ya washindi hao, watatu walijishindia simu janja, wengine watatu walijishindia televisheni za kisasa na mmoja alijishindia pikipiki. Washindi hao wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao tarehe 18 mwezi huu. Promosheni ya Kapu la Wana ilizinduliwa tarehe 02 mwezi wa pili. Droo inayofuata itakuwa ya mwisho ambapo zawadi kubwa ya gari itapatikana.


Mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania Salim Mgufi (kushoto) akizungumza jambo wakati wa droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Masoko wa Serengeti Breweries, Emila Tom Machuve.

No comments:

Post a Comment