Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 21 March 2023

RAIS SAMIA AIPONGEZA BENKI YA TADB NA KUSISITIZA KUENDELEA KUWEZESHA MRADI WA BBT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Frank Nyabundege (wa kwanza kulia) wakati wa uzinduzi wa Mashamba Makubwa ya Pamoja (Block Farming) uliofanyika Chamwino, Dodoma. TADB iliwapatia washiriki 812 wa Programu ya Kilimo Biashara - Building a Better Tomorrow (BBT) zana na vitendea kazi vya kilimo vyenye thamani ya Shilingi Milioni 500. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kazi nzuri inayoifanya na kuiasa kuendelea kuwezesha Programu ya Vijana ya Kilimo Biashara 'Building a Better Tomorrow' (BBT) kwa kupatia washiriki wake zana na vitendea kazi vya kilimo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo wa programu hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Frank Nyabundege (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana ambao ni washiriki wa Programu ya Kilimo Biashara - Building a Better Tomorrow (BBT) muda mfupi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzindua programu hiyo Chamwino, Dodoma. TADB imetoa zaidi ya Shilingi Milioni 500 kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na program hiyo kwa awamu hii ya kwanza.

Rais Samia alitoa pongezi hizo wakati akikagua zana na vitendea kazi vya kilimo vilivyotolewa na TADB Chinangali, Wilaya ya Chamwino kwa ajili ya uzinduzi wa Mashamba Makubwa ya Pamoja (Block Farming) iliyo chini ya programu hiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana ambao ni washiriki wa Programu ya Kilimo Biashara 'Building a Better Tomorrow' (BBT) muda mfupi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzindua programu hiyo Chamwino, Dodoma. TADB imetoa zaidi ya Shilingi Milioni 500 kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na program hiyo kwa awamu hii ya kwanza.

TADB imetoa zaidi ya Shilingi Milioni 500 kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na programu hiyo kwa awamu hii ya kwanza.

No comments:

Post a Comment