Mwenyekiti Wa Klabu ya Lugalo Gofu, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo (katikati), Katibu wa Klabu hiyo, Luteni Kanali Shabani Kitogo(kulia) na Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto) wakikabidhi zawadi ya baiskeli kwa mshindi wa kwanza upande wa watoto (Juniors) katika Shindano la "NBC Lugalo Open 2023" , Omari Shabani. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa Mashindano wa Chama Cha Mchezo wa Gofu Tanzania TGU, Ernest Sengeu.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma akicheza mchezo wa Gofu katika kufunga mashindano ya NBC Lugalo Open 2023 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Jeshi vya Gofu Lugalo, Dar es Salaam mwishoni wa wiki iliyopita. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa benki ya NBC, James Meitaron na Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo, Brigedia Generali mstaafu Michael Luwongo.
Dar es Salaam, Machi 27, 2023: Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ameipongeza Benki ya NBC kutokana na jitihada zake za kusaidia maendeleo ya michezo mbali mbali nchini.
Akizungumza wakati hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa gofu wa NBC Lugalo Open 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Jeshi Lugalo, Mh. Mwinyijuma alisema benki ya NBC imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika sekta michezo hapa nchini na kuongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa benki hiyo. “Nikiwa kama Naibu Waziri mwenye dhamana ya Utamaduni, Sanaa na Michezo napenda kuishukuru benki ya NBC kwa kutuunga mkono katika jitihada za kuendeleza na kukuza maendeleo ya michezo.
Akizungumza wakati hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa gofu wa NBC Lugalo Open 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Jeshi Lugalo, Mh. Mwinyijuma alisema benki ya NBC imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika sekta michezo hapa nchini na kuongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa benki hiyo. “Nikiwa kama Naibu Waziri mwenye dhamana ya Utamaduni, Sanaa na Michezo napenda kuishukuru benki ya NBC kwa kutuunga mkono katika jitihada za kuendeleza na kukuza maendeleo ya michezo.
NBC imekuwa ikifadhili michezo mbali mbali kiwa ni pamoja na ligi ya Kuu ya Tanzania bara, Dodoma Marathon n.k. Ligi yetu kwa sasa ni moja ya ligi zinazotajwa kuwa ni ligi bora barani Afrika na hii imewezekana kutokana na mchango wabenki ya NBC,” alisema Mhe. Mwinjuma.
Aliongeza: “Ni rai yangu kwa NBC kuendeleza kuweka mkono kwenye michezo yetu na kwenye sehemu nyingine za kijamii hapa nchini. Makampuni na taasisi nyingine pia ziige wanachokifanya benki ya NBC ili tuweze kupiga hatua kubwa na kwa haraka zaidi,” Naibu Waziri aliipongeza NBC kufadhili michezo mbali mbali “Sikutegemea kuwakuta kwenye gofu, nimefurahishwa na jitihada zenu kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuimarisha michezo Tanzania. Hongereni sana NBC nyinyi ni mfano wa kuigwa,” aliongeza Mhe. Mwinjuma.
Aidha, Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa benki hiyo Bw. James Meitaron alisema kuwa kupitia sera ya kurudisha kwa jamii, benki hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali kuendeleza na kukuza michezo mbali mbali nchini. “Tunaamini kuwa ushiriki wetu kwenye eneo hili la michezo pamoja na kusaidia juhudi za serikali katka maeneneo mengine, utasaidia kuboresha maisha ya Wanzania ikiwa pia ni sehemu yetu ya kurudisha kwa jamii . Kama tulivyoahidi hapo awali, leo tumetoa tuzo mbali mbali kwa washiriki wa mashindano haya ya wazi ya NBC Lugalo 2023 yaliyoanza jana,” alisema Bw. Meitaron.
Kwa upande, mshindi wa kwanza wa mashindano hayo Bw. Ally Mcharo aliishukuru benki ya NBC kwa kudhamini na kufanikisha mashindano na pia aliushukuru uongozi wa Klabu ya Gofu ya Lugalo kwa kukubali kufanya mashindano hayo na kuwapa fursa vijana kuweza kuonyesha vipaji vyao.
No comments:
Post a Comment