Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 14 March 2023

MKURUGENZI MKUU WA NHC AJITAMBULISHA RASMI KWA UONGOZI WA WIZARA YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, akiagana Mkurugenzi Mkuu Bw. Hamad Abdallah mara baada ya mazungumzo yao ya kikazi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa - NHC Bw. Hamad Abdallah (kulia) akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Ardhi, Geofrey Pinda (kushoto) na Katibu Mkuu, Mhandisi Anthony Sanga mara baada ya kuwasili ofisini kwa Naibu Waziri.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akimweleza jambo Mkurugenzi Mkuu Bw. Hamad Abdallah mara baada ya kuwasili ofisini kwa Katibu Mkuu huyo.

Mkurugenzi Mkuu Bw. Hamad Abdallah akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Viongozi wa Wizara ya Ardhi wakiwa na Mkurugenzi Mkuu katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa NHC.

Naibu Waziri wa Ardhi, Bw. Geofrey Pinda akiagana na Mkurugenzi Mkuu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa - NHC Bw. Hamad Abdallah leo amekutana na uongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi jijini Dodoma kama sehemu rasmi ya kujitambulisha.

Pamoja na kujitambulisha pia Mkurugenzi Mkuu Bw. Abdallah ameuelezea uongozi wa Wizara muelekeo wa utendaji wake namna utakavyokuwa na kupokea maoni ya Wizara namna inavyotarajia kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa.

Katika mazungumzo yao viongozi wa Wizara wamelipongeza Shirika kwa kazi nzuri inazozifanya na kuahidi kuendelea kumpa ushirikino Mkurugenzi Mkuu mpya ili hatimaye NHC iweze kubadili miji na kuwa na makazi bora.

“Wizara iko tayari kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu ili kulisaidia Shirika kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwani Watanzania wanalitegemea sana Shirika kwa kuwapatia makazi bora na kwamba NHC ihakikishe inakamilisha miradi yake kwa wakati na kubuni miradi mipya itakayoliletea Shirika faida” Alisema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula.

Dkt. Mabula ameongeza kusema kuwa Wizara inalitegemea sana Shirika kuweza kupata maoni yenye kuleta ubunifu wa namna ya kuboresha miji yetu, kuipanga upya na kuondoa makazi holela.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Abdallah ameushukuru uongozi mzima wa Wizara kwa kuupokea vyema uongozi wa NHC na amehaidi kushirikiana na Wizara na Serikali kwa ujumla katika kuhakikisha kwamba Shirika linatekeleza kazi zake kwa ufanisi ili kukidhi matarajio ya watanzania.

Katika kikao kilichoongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula, pia kilihudhuriwa na Naibu wake Geofrey Pinda na Katibu MKuu wa Wizara hiyo Mhandisi Athony Sanga.

Bw. Hamad Abdallah amekutana na uongozi wa Wizara ya Ardhi kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuliongoza Shirika la Nyumba la Taifa Februari 24 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment