Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 1 March 2023

MKURUGENZI MKUU HAMAD ABDALLAH AKABIDHIWA RASMI MIKOBA YA NHC

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah akipeana mkono na Msajili wa Hazina, Nehemia Kyando Mchechu ikiwa ni ishara ya makabidhaino rasmi ya Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Kambarage House Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah akiendelea na taratibu za makabidhiano na Msajili wa Hazina, Nehemiah Kyando Mchechu kwenye ofisi za NHC Kambarage House Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah amewasili na kukabidhiwa rasmi ofisi Februari 28, 2023 na mtangulizi wake, Nehemiah Kyando Mchechu ambaye ameteuliwa na Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Msajili wa Hazina.

Makabidhiano hayo yamefanyika Ofisi za NHC Kambarage House Jijini Dar es Salaam baaada ya viongozi hao wawili kuwasili Ofisini wakitokea Jijini Dodoma waliokwenda kuapa kiapo cha utii kwa Jamhuri.

Aliyetangulia kuwasili alikuwa ni Msajili wa Hazina ambaye ndiye Mkurugenzi Mkuu anayeondoka na kufuatiwa na Mkurugenzi Mkuu mpya Hamad Abdallah wakafika ofisini, kutia saini katika kitabu cha wageni na kuwa na kikao cha pamoja baina yao, baadaye wakakutana na Menejimenti ya NHC na hatimaye kukutana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa.

Viongozi wote wawili walipowasili kwa nyakati tofauti walipokelewa kwa bashasha na wafanyakazi wa Shirika wakiwamo Menejimenti na baadhi ya wafanyakazi walioteuliwa kuwawakilisha wenzao.

Ijumaa Februari 24, 2023, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan alimteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Kyando Mchechu kuwa Msajili wa Hazina.

Kufuatia uteuzi huo, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akamteua Hamad Abdallah kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuanzia Ijumaa.

Hamad Abdallah amewahi kuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa kati ya mwaka 2010 mpaka mwaka 2018. Kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kushika wadhifa huu mpya Hamad Abdallah alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited.

Nehemiah Mchechu aliliongoza Shirika la Nyumba la Taifa tangu mwaka 2010 mpaka 2018 na aliteuliwa tena na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 14, 2022 kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC.

Hamad anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa 13 wa Shirika la Nyumba la Taifa lililoasisiwa na Muasisi wa Taifa hili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na amechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio la Shirika hili lenye mtaji wa Shilingi trilioni 5.04 kutoka Shilingi trilioni 1.5 mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment