Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Thursday, 2 March 2023
KAMPUNI YA TATU KUTANGAZWA WASHINDI WA PROGRAMU YA VODACOM DIGITAL ACCELERATOR
Dar es Salaam – Machi 1, 2023: Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC inatarajia kutangaza kampuni bunifu chipukizi tatu zilizoibuka washindi wa msimu wa pili wa programu ya Vodacom Digital Accelerator iliyofanyika kwa kushirikiana na Smart Lab.
Washindi watapatikana baada ya kuwasilisha na kuonyesha shughuli wanazozifanya kwa jopo la majaji waliobobea kwenye maeneo ya teknolojia, ujasiriamali, uwekezaji, na sheria. Uwasishaji wa maonyesho hayo unatarajiwa kufanyika siku ya Machi 3, katika hoteli ya Hyatt Regency ya jijini Dar es Salaam.
Ikiwa imebuniwa kwa ajili ya kampuni bunifu chipukizi zinazoamza kujiendesha kwa faida, msimu wa pili wa programu ya Vodacom Digital Accelerator ulianza mwezi Aprili mwaka 2022 na kuruhusu maombi kutoka kwa kampuni zote bunifu chipukizi za kiteknolojia za Kitanzania zenye mustakabali wa kukua. Kutoka mamia ya maombi yaliyopokelewa, kampuni 12 zilichaguliwa kujiunga na programu hii na kuingia kwenye hatua ya kujengewa uwezo ambapo zilipatiwa msaada wa ziada kwenye kukuza mikakati yao ya kimasoko, eneo la kiufundi, na kuwaunganisha kwa washirika na wawekezaji.
Kampuni hizo bunifu chipukizi zinatoka kwenye sekta tofauti ambazo ni Pamoja na huduma za kiteknolojia za kifedha, afya, biashara za mtandaoni, elimu, kilimo, na usalama wa mtandaoni.
“Tumefurahi kufikia hatua hii ya programu yetu ya Vodacom Digital Accelerator ambapo tumefanikiwa kuona namna ilivyosaidia kukuza ubunifu kwa kampuni chipukizi za Kitanzania, uwasilishaji tutakaojionea kwenye maonyesho ndio utasaidia kuwatambua washindi watatu, ambao watazawadiwa Zaidi ya Shilingi milioni 200 za Kitanzania za msaada wa kulingana na thamani Pamoja na uwezekano wa uwekezaji zaidi mbeleni. Ningependa kutoa wito kwa wadau kwenye sekta ya ubunifu na teknolojia kujisajili kwa njia ya mtandaoni ili kushiriki wakiwa popote walipo siku ya kesho,” alisema Bw. Nguvu Kamando, Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali, Vodacom Tanzania PLC.
Watu wote wanakaribishwa kujiunga nazi, au kusikiliza uwasilishaji wa maonyesho hayo na kuweza kuzipigia kura kampuni bunifu chipukizi bora kupitia kiambatanisho (link) ambacho kitapatikana kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya kampuni.
Kampuni bunifu chipukizi ambazo zimefikia hatua ya fainali ni pamoja na Shule Yetu Innovations, Smart Darasa, Lango Academy, na Vijana Tech, kwa upande wa huduma za elimu za kiteknolojia. Hack it Consultancy inawakilisha eneo la huduma za usalama wa mtandaoni. Seto, Twenzao, Get Value, na Spidi Africa zipo chini ya biashara za mtandaoni. Nyinginezo ni Medpack ikiwakilisha huduma za afya za kiteknolojia, zikiwemo na, Bizy Tech Pamoja na Bizzy Pay ambazo zenyewe zipo upande wa huduma za kifedha za kiteknolojia.
About Vodacom Tanzania:
Vodacom Tanzania Plc is the country’s leading mobile operator and mobile financial services provider. We provide a wide range of communication services for consumers and enterprise – including voice, data and messaging, video, cloud and hosting, mobile solutions, and financial services – to over 17 million customers. Vodacom Tanzania Plc and its subsidiary companies are part of the Vodacom Group registered in South Africa, which is in turn owned by Vodacom Group Plc of the United Kingdom. It has been registered on the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) with registration number ISIN: TZ1886102715 Stock name: VODA.
For further information please visit our website: www.vodacom.co.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment