- Sasa wateja wanaweza kutumia mpaka laini tano kwenye simu moja tu!
“Airtel eSIM inakuja na faida nyingi ikilinganisha na laini za kawaida zikiwemo hizi;
- eSIM ni haraka na rahisi kuunganishwa mtandaoni.
- Ukiwa na eSIM, mteja anaweza kutumia hadi laini tano hivyo kuepuka mzigo usio wa lazima wa kubeba zaidi ya simu moja
- eSIM inaweza kuunganishwa na iWatch yako wakati ambapo unafanya mazoezi iwe marathon au GYM unaendelea kuwa umeunganishwa na mtandao
- Laini ya eSIM ni salama Zaidi – kwa kuwa huwezi kupoteza laini hiyo bila kupoteza simu yako kwani wote tunafahamu laini za kawaida kuna muda huwa zinapotea, kuibiwa na kutumika kwenye utapeli
- eSIM ni rafiki wa Mazingira kwa kuwa hakuna vile viambata vya plastiki wala vibati vinavyotolewa ukiwa unanunua laini yako ya eSIM.
- Ikiwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara nje ya nchi eSIM itakuwa ni rahisi kwako kubadilisha mtandao ukiwa popote
“Angalizo ni kwamba sio simu zote zina uwezo wa kutumia eSIM. Baadhi ya Simu zinakubali Matumizi ya eSIM ni Pamoja na, IPHONE , SAMSUNG, GOOGLE PIXEL na MOTOROLA Piga *#06# kuhakiki uwezo wa SIMU yako kisha angalia EID. alisema Singano huku akisisitiza kuwa faida kubwa ya kuwa na eSIM swala la Usalama, kwamba huwezi kupoteza laini hiyo bila kupoteza simu yako kuna ugumu wa mtu kucheza na taarifa ukiwa eSIM”.alieleza Singano
Airtel itaendelea kutambulisha bidhaa na huduma mpya za kusisimua kwa wateja wake huku tukihakikisha huduma bora na nafuu kwa wakati wote. Matarajio na mahitaji ya wateja wetu yanabadilika na Airtel tuna uhakika kwamba wateja wetu watahamia kwenye laini za eSIM kulingana na faida zake kwenye matumizi. Ni Imani yetu kuwa wateja wetu na Watumiaji wa eSIM watafurahia ubunifu huu wa kidigitali. aliongeza Singano.
Msanii wa kizazi kipya maarufu kama Diamond Platnumz na ambaye pia ni balozi wa Kampuni ya Airtel aliipongeza Kampuni hiyo kwa kuwa ya kwanza kuleta kwenye teknolojia ya eSIM huku akiahidi kuendelea kupeperesha bendera vizuri kwa kutangaza bidhaa na huduma za Airtel.
“Ninayo furaha kuwa kwenye Kampuni hii ambayo inathamini sana bidhaa zenye bunifu na kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja wake. Ukiwa na eSIM kutoka Airtel Tanzania sasa hakuna sababu ya kutembea na mzigo mkubwa wa simu kwani ili uwe umeunganishwa na laini zako, ukiwa na eSIM unaweza kutumia hadi laini tano kwenye simu moja”.
Ili kupata ESIM, tembelea kwenye duka lolote la Airtel nchini ambapo watoa huduma wetu atakuongoza kwenye mchakato mzima wa kubadilisha laini yako ya kawaida au na kupata laini mpya ya kidigitali ya eSIM.
No comments:
Post a Comment