Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba, amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na Benki ya Dunia ili kuharakisha maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii.
Dkt. Mwamba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia, Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe, aliyefika Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kujitambulisha.
Alisema kuwa mazungumzo yao yalilenga kuchambua fursa zinazopatikana kwenye Benki ya Dunia ambazo Tanzania kama Mwanahisa inaweza kuzifikia na kuzitumia kwa ajili ya maendeleo ya nchi na watu wake.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayesimamia maslahi ya nchi 22 za Kanda Namba Moja Afrika kwenye Taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani, Dkt. Zarau Kibwe, alisema kuwa majadiliano yao yamekuwa na mafanikio makubwa.
Hii ni mara ya kwanza kwa Viongozi hao kukutana kikazi baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba kuteuliwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushika wadhifa wa Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment