Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Timu ya Yanga, Andre Mtine (wa pili kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Timu ya Simba, Imani Kajura (wa pili kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa makubaliano wa kuwatumia wachezaji Clatous Chama, Mohammed Hussein, Aziz Ki na Farid Mussa kutoka timu za Simba na Yanga kuwa mabalozi wa Benki ya CRDB katika kufikisha elimu ya fedha kwa jamii kupitia kampeni yake ya “Benki ni SimBanking”. Hafla ya kusaini mikataba hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam. Wa pili kulia waliosimama ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda pamoja na wanasheria Hosea Samba (Timu ya Simba) , Simon Patrick (Yanga) na Danford Kisinda wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela amesema Benki ya CRDB kwa muda mrefu imekuwa ikishiriki katika kusaidia jitihada mbalimbali za kimichezo kwa kutambua mbali ya kuwa michezo ni burudani, bali pia michezo ni biashara na uchumi pia.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Benki ya CRDB imeanzisha mbio za kimataifa za hisani za CRDB Bank Marathon, mashindano ya taifa ya mpira wa kikapu ya CRDB Bank Taifa Cup pamoja na mashindano ya resi za Ngalawa ya CRDB Bank Ngalawa Race.
Benki ya CRDB imefikia hatua ya kusaini makubaliano na wachezaji hao wa Simba na Yanga ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza wigo wa ufahamu wa elimu ya fedha kwa wachezaji wa soka na jamii kwa ujumla lakini pia ikiwa ni sehemu ya kutambua viwango vizuri ambavyo vimeonyeshwa na wachezaji hao katika kusaidia timu zao kupata matokeo mazuri lakini pia nidhamu ambayo wameonyesha katika mchezo jambo ambalo ni muhimu sana kwa mafanikio ya mchezaji.
“Tunaishukuru Benki ya CRDB kwa kuwatambua wachezaji wetu na kuwapa heshima hii kubwa ya kuwa mabalozi wao. Kwa kuwa mabalozi wa taasisi kubwa kama Benki ya CRDB kunaleta imani na hamasa hata kwa taasisi nyingine kutaka kushirikiana na wachezaji wetu jambo ambalo litanuifaisha sio tu wachezaji bali vilabu na soka letu kwa ujumla wake” alsema Mtine.
“Pamoja na kuwa mikataba hii inakwenda kuongeza kipato kwa wachezaji lakini kupata nafasi ya kupewa elimu ya fedha ambayo itawasaidia kwenye maisha yao wakati huu wanacheza soka la ushindani na wakati ambao watakua wamestaafu ni jambo kubwa na la kupongezwa kwani wachezaji wengi wameshindwa kunufaika na vipaji vyao kwa kukosa elimu ya fedha” aliongeza Kajula ambae amewahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za fedha nchini.
No comments:
Post a Comment