Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema ushirikiano na taasisi hizo za Serikali utasaidia kufanikisha malengo ya programu kwa kiasi kikubwa kutokana na jinsi uzoefu wa taasisi hizo katika kuwawezesha vijana wabunifu katika sekta mbalimbali.
ICTC na COSTECH wamekuwa wakifanya kazi nzuri ambayo inaakisi utayari wa Serikali yetu katika kukuza biashara na mawazo ubunifu, hivyo tunajivunia kwa hatua hii muhimu,” alisema.
Katika hafla hiyo, Benki ya CRDB pia iliutangazia umma kuanzishwa kwa taasisi isiyo ya faida ya “CRDB Bank Foundation” yenye jukumu la kuanzisha na kutekeleza programu bunifu, endelevu, na shirikishi zinazolenga kuleta ustawi wa kijamii, na kiuchumi kama ‘IMBEJU’.
Akizungumza kwa mara ya kwanza kama Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Bank Foundation, Mwambapa amewataka vijana wabunifu kuchangamkia fursa inayotolewa na benki hiyo kupitia programu ya IMBEJU inayotekelezwa kwa kushirikiana na ICTC, na COSTECH.
Mwambapa alitumia fursa hiyo pia kuwaalika vijana kushiriki semina maalum ya uwezeshaji iliyoaandaliwa na Benki ya CRDB tarehe 11 Machi 2023 katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere, ambapo programu hiyo itaingizwa sokoni rasmi, na uwezeshaji kuanza kufanyika. Mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
No comments:
Post a Comment