Baadhi ya wageni waliotembea banda la maonyesho la Bank of Africa, wakipatiwa maelezo ya huduma zinazotolewa na benki kutoka kwa Wafanyakazi wa Benki hiyo. |
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Adam Mihayo, wakati akieleza ushiriki wa Benki hiyo katika Jukwaa la biashara la Tanzania na nchi za Ulaya (EU-Tanzania Business Forum) lililomalizika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
“Huu ni moja ya mkakati mkuu wa Benki yetu wenye lengo la kuunga mkono dira ya Serikali ya Tanzania katika ajenda ya ujumuishaji katika mfumo rasmi wa kifedha hususani katika makundi ya biashara ndogo na za kati na uwezeshaji wa Wanawake”, alisema.
Mihayo, alisema kuwa Bank of Africa, imekuwa na programu ya kuwapatia wafanyakabiashara wadogo na wa kati (SMEs) mafunzo ya uendeshaji biashara zao kwa ufanisi sambamba na kuwapatia mikopo kw ajili ya kukuza biashara zao.
Mkutano wa Jukwaa la Biashara la EU-Tanzania ulilenga kuonyesha fursa za biashara zilizopo nchini Tanzania na kueleza mikakati ya kufanikisha uwekezaji wa kibiashara kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ulaya na Tanzania.
Bank of Africa, kupitia huduma zake bora na mtandao wake thabiti katika nchi 18 za Afrika imedhamiria kuendelea kufanikisha ushirikishwaji wa kifedha kupitia ubia na ushirikiano.
No comments:
Post a Comment