Kutoka kushoto ni Mwanasheria anayeiwakilisha HAIER, Beauttah Camara, Mwakilishi wa HAIER Tanzania, Leon Chi, Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said na Mwanasheria anayeiwakilisha Yanga, Simon Patrick. |
HAIER ni kampuni namba moja kwa kutengeneza bidhaa bora za umeme majumbani na ofisini, ikiwa na tuzo Zaidi ya 500 za ubunifu zenye kuzingatia teknolojia bora na rahisi kwa mtumiaji.
Mwakilishi wa HAIER Tanzania, Leon Chi. |
Mkataba huu umesainiwa na Rais wa Klabu ya Yanga, Eng Hersi Said pamoja na mwakilishi wa kampuni ya HAIER, Leon Chi, kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Serena Hotel, Dar Es Salaam.
HAIER ambao bidhaa zao kwa hapa Tanzania zitasambazwa na kampuni ya GSM Group, itawekwa mbele kwenye jezi za Yanga watakazotumia kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho la CAF pamoja na kupata nafasi kwenye mitandao yetu ya kijamii.
Rais wa Klabu ya Yanga, Eng Hersi Said.
Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said amesema ni jambo kubwa kwa klabu ya Yanga kusaini mkataba na Kampuni hii kubwa duniani.
“Young Africans SC imeingia mkataba na kampuni ya Haier wenye thamani ya Tsh bilion 1.5 kama mdhamini mkuu wa Kombe la shirikisho barani Afrika,” Rais Hersi Ally Said
Naye mwakilishi wa HAIER, Leon Chi amesema wamevutiwa kufanya kazi na Yanga kwa sababu ndio klabu yenye mafanikio Zaidi hapa Tanzania, ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara 28, mataji mawili ya Kombe la Shirikisho la AZAM na makombe sita ya Ngao ya Jamii lakini pia imefanikiwa kutengeneza rekodi kubwa ya Unbeaten kwenye historia ya CAF.
“Hatupo Tazania kwa ajili ya biashara tu bali pia kusaidia jamii kubwa ya vijana wenye vipaji kupitia mchezo wa mpira wa miguu. Tunafuraha kubwa kushirikiana na timu hii iliyopata ushindi wa kihistoria nchini Tunisia dhidi ya Club Africain.
“Tuna Imani kubwa na mshirika wetu GSM Group kuwa msimu huu pia Yanga itabeba ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya 29 na kufanya vizuri Zaidi kwenye michuano ya kimataifa,” alisema Leon.
No comments:
Post a Comment