Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 15 November 2022

DCB YASHINDA TUZO YA BENKI BORA KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA NCHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza muda mfupi baada ya benki hiyo kutangazwa mshindi wa kwanza wa Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora kwa Wateja Nchini ya Tuzo za Chaguo la Mlaji Afrika (CCAA) kwa mwaka 2022 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya DCB, Dk. Amina Baamary (wa tano kushoto), akipokea tuzo ya mshindi wa kwanza ya Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora kwa Wateja nchini kwa mwaka 2022 katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa Tuzo za Chaguo la Mlaji Afrika (CCAA) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya DCB, Dk. Amina Baamary (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa (wa nne kushoto), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakishangilia mara baada ya kupokea tuzo ya mshindi wa kwanza ya Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora kwa Wateja nchini kwa mwaka 2022 katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa Tuzo za Chaguo la Mlaji Afrika (CCAA) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Benki ya Biashara ya DCB imesema ushindi wa benki bora katika utoaji huduma kwa benki zenye ukubwa wa kati ilioupata, umetokana na mabadiliko makubwa iliyoyafanya katika mfumo mzima wa utoaji wa huduma kwa wateja wao.

Akizungumza katika hafla za utoaji zawadi za Tuzo za Chaguo la Mlaji Afrika (CCAA) jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema ushindi huo uliotokana na uboreshaji mkubwa walioufanya katika huduma zao umekuja kwa wakati mzuri kipindi hiki DCB ikisherehekea miaka 20 tokea ilipoanzishwa.

“Kwa niaba ya familia ya DCB, napenda kushukuru sana wateja wetu na wasio wateja wetu kwa kutupigia kura kwa kuwa benki bora kabisa nchini kwa kutoa huduma bora, kupata tuzo hii kunazidisha furaha yetu wakati tukiendelea kusherehekea miaka 20 ya benki yetu.

“Mimi na wafanyakazi wenzangu tunafuraha kuona wateja wetu wameweza kuona uboreshaji mkubwa tulioufanya wa jinsi tunavyowahudumia, hii ni safari tuliyoanza miaka minne iliyopita na tunashukuru kuona matunda yake yanaonekana na wateja wameweza kuyaona,” alisema Bwana Ndalahwa.

Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mafanikio hayo wao kama wanafamilia wa DCB wanayachukulia kama changamoto ya wao kuzidi kuboresha zaidi huduma zao na kuwa zaidi ya mahali walipo.

Hii ni mara ya pili kwa DCB kushinda tuzo hii japo kwa mara ya kwanza mwaka 2021 ilitwaa ushindi wa pili wa tuzo hizi zenye lengo la kuleta ushindani kati ya makamapuni na biashara mbali mbali barani Afrika, kuhamasisha utoaji huduma na bidhaa bora kwa wateja pamoja na kutambua kazi bora za watoa huduma.

No comments:

Post a Comment