Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 25 October 2022

DSTV PEKEE KUONYESHA MECHI ZOTE 64 ZA KOMBE LA DUNIA LA FIFA 2022


SuperSport International (Pty) Limited, moja ya kampuni tanzu ndani ya Kundi la Makampuni ya MultiChoice inayowakilishwa hapa nchini na kampuni ya MultiChoice Tanzania Limited, imbainisha kuwa ina haki za kipekee za matangazo kwa Televisheni za kulipia (exclusive Pay Tv broadcast rights) ya mashindano ya FIFA WORLD CUP 2022kitendo ambacho kinaifanya SuperSport kuweza kuonyesha mbashara mechi zote 64 za mashindano hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na MultiChoice Tanzania, matangazo ya aina hiyo ya mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 yanaruhusiwa kurushwa kupitia Chaneli za SuperSport pekee ambazo hupatikana katika kisimbuzi cha DStv. Kwa mujibu wa taarifa hiyo haki hizi ni kwa ukanda wote wa Afrika – Kusini mwa Jangwa la Sahara na visiwa jirani (Sub-Saharan Africa and adjacent islands) ikiwemo Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika kuhakikisha kuwa wateja wa DStv wanafurahia vizuri zaidi mashindano hayo ya Kombe la Dunia, SuperSport imetenga chaneli mahsusi kwa ajili ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 20 hadi Desemba 18 mwaka huu huko nchini Qatar. Kutengwa kwa chaneli hizo kutawawezesha watazamaji wa DStv kuona mechi hata zile ambazo zitachewa kwa wakati mmoja mechi zaidi ya moja.

Kwa msingi huo ni wateja wa DStv pekee ndiyo wataweza kushuhudia mechi zote 64 za michuano hiyo mbashara kupitia chaneli za SuperSport.

Ili kuhakikisha kuwa wateja wa DStv hawapati usumbufu, zimetengwa chaneli mbili mahususi FIFA World Cup central na FIFA World Cup Africa kwa ajili ya michuano hiyo ambapo chaneli hizo muda wote zitakuwa zikionyesha matukio mbalimbali yanayouhsiana na mashindano hayo ikiwemo uchambuzi wa wataalamu wa soka, Makala za matukio muhimu katika mashindano yaliyopita Pamoja na kurusha mbashara mechi zote

No comments:

Post a Comment