Waziri Mkuu aliyasema hayo katika hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Balozi Paul Rupia katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam na baadae kufuatiwa na maziko yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini humo.
Waziri Mkuu alisema moja ya jambo ambalo halitasahaulika kwa Marehemu Balozi Paul Rupia ni mchango wake mkubwa kwa benki hiyo kwani hadi anaondoka katika Uongozi aliiacha benki hiyo ikiwa na matawi nane.
“Mheshimiwa Rais Samia amenituma kuja kumuwakilisha katika msiba huu, amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo za Balozi Rupia, hakuweza kuhudhuria kwa sababu yupo nchini Msumbiji kwa ziara ya kikazi, pia ametoa pole kwa familia na waombolezaji wote”, alisema Waziri Mkuu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Zawadia Nanyaro alisema, benki ilipata mshtuko na masikitiko makubwa mara baada ya kupata taarifa za kifo cha Mwenyekiti huyo wa kwanza wa benki hiyo, Balozi Paul Rupia.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na viongozi wengine wa kiserikali na kisiasa alisema Marehemu Balozi Paul Rupia aliivusha benki katika vipindi muhimu vya hatua za ukuaji wa benki tokea mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya DCB mnamo Mwaka 2000 hadi inaanzishwa rasmi mwaka 2002.
“kwa kipindi cha miaka 15 cha uongozi wake, Marehemu Balozi Rupia alifanikisha hatua mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na benki kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), na pia kubadilika kwa benki kutoka kuwa Benki ya Watu wa Dar es Salaam na kuwa Benki ya Biashara ya DCB.
“Wakati DCB ikiendelea kusherehekea miaka 20 tokea ilipoanzishwa, mchango wa marehemu Balozi Paul Rupia hautaweza kusahaulika, kwani aliiongoza benki kwa weledi mkubwa na alihakikisha benki inakuwa kimtaji na kuongeza matawi kutoka moja hadi nane alipostaafu”, aliongeza Bi. Zawadia.
Aidha mwenyekiti huyo alisema, Marehemu Balozi Rupia hata baada ya kustaafu kwake aliendelea kushirikishana na DCB akiwa pia mmoja wa wanahisa waanzilishi wa benki hiyo na wakati benki ikiadhimisha miaka 20 Mwezi Mei, licha ya kukabiliwa na matatizo ya kiafya, Balozi Rupia alikubali kushiriki sherehe hizo kwa njia ya video.
“Tutaendelea kuenzi yale yote mema aliyoyafanya katika benki yetu, nasi tunaungana na waombolezaji wengine kuwapa pole wanafamilia na viongozi wote kwa msiba huu uliotufikia na tunaendelea kuiombea roho ya marehemu ipumzike kwa amani”, alisema.

No comments:
Post a Comment