Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 13 September 2022

SERIKALI YAIMWAGIA SIFA VODACOM KUBORESHA MAKAZI

Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya (kushoto), Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Nehemiah Mchechu, akimkabidhi mfano wa ufunguo, Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano na Teknolojia ya Vodacom, Kanda ya Kati - Joseph Sayi, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Iyumbu, Dodoma, katika mradi wa Nyumba 300 unaotekelezwa na NHC mahala hapo, Vodacom, imenunua nyumba hiyo kwa gharama ya shilingi milikoni 102, kwa ajili ya mshindi wa droo yake iliyofikia tamati ya Mpesa Imetiki.

Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya (katikati), akimkabidhi mfano wa ufunguo, Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano na Teknolojia ya Vodacom, kanda ya Kati Joseph Sayi, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Iyumbu, Dodoma, katika mradi wa Nyumba 300 unaotekelezwa na NHC mahala hapo, Vodacom, imenunua nyumba hiyo kwa gharama ya shilingi milikoni 102, kwaajili ya mshindi wa droo yake iliyofikia tamati ya Mpesa Imetiki. Kushoto ni Meneja Mauzo na Masoko wa NHC, Itandula Gambalagi.

Serikali imeipongeza Kampuni ya Mawasiliano na Teknolojia ya Vodacom kwa kuunga mkono azma ya Serikali ya kuondoa ombwe la makazi nchini kwa kuwapatia wananchi nyumba bora

Wito huo umetolewa jijini Dodoma Septemba 5, 2022, na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi, wakati wa hafla fupi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuikabidhi Kampuni ya Mawasiliano na Teknolojia ya Vodacom.

Mshindi wa zawadi ya nyumba ya Droo ya Vodacom ya Mpesa imetiki, bi Rahabu Jackson, mkazi wa Manyoni, Singida, akiwa mezani kwake na Mgeni rasmi Dkt Kijazi na Viongozi wa NHC na Vodacom.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia kampuni hiyo kununua nyumba kutoka NHC, katika mradi wa nyumba 300 wa Iyumbu, yenye thamani ya Shilingi Milioni 102, kisha Vodacom, kuikabidhi kwa mshindi wa Droo yake ya Mpesa imetiki.

Dkt. Kijazi,amesema Vodacom walikuwa na uwezo wa kwenda kununua nyumba mahala popote, kwa bei ya chini tena isiyo katika makazi endelevu, lakini kitendo cha kununua nyumba kwa Shirika la Nyumba la Taifa, ni kitendo kilichoitia moyo Serikali kupitia NHC.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi, wakati wa hafla fupi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), akikabidhi ufunguowa nyumba kwa Kampuni ya Mawasiliano na Teknolojia ya Vodacom ili imkabidhi mshindi wa zawadi ya nyumba wa Droo ya Vodacom.

"Sisi Serikali tuko tayari kuwa na ushirikiano endelevu hususani pale Vodacom na wengine wakiwa tayari kuunga mkono azma ya serikali ya kuondoa ombwe la makazi nchini, kwa kuwapatia wananchi nyumba bora na ndiyo maana nimesema, Wizara imefurahishwa sana na uungwaji mkono huo wa Vodacom."

Dkt. Kijazi amechukua fursa hiyo kuwashukuru NHC, kwa kuwa na ubunifu na kuja na mradi huo wa Iyumbu, na ana imani kupitia tukio la leo, litasaidia kuonyesha Watanzania, kazi nzuri inayofanywa na Shirika lao la nyumba, katika kuhakikisha kwamba Watanzania, wanakuwa na makazi bora lakini pia wanapata nyumba za bei nafuu.

Naye Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano na Teknolojia ya Vodacom, kanda ya Kati, Joseph Sayi, alisema, mojawapo ya sababu za Vodacom, kununua nyumba kutoka NHC ni ukongwe walionao katika sekta ya nyumba lakini pia upekee walionao katika sekta hiyo.

"NHC ni Shirika bobezi katika sekta ya nyumba, linaaminika, lakini kubwa zaidi ni weledi wake katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nyumba nchini, hivyo kwa vigezo hivyo vilitufanya Vodacom tusishikwe na kigugumizi kufanya maamuzi ya kununua nyumba kutoka shirika hilo,’’ alisema Mkuu huyo wa Vodacom kanda ya kati, Joseph Sayi.

Awali Meneja Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, mbali na kuishukuru Vodacom, kwa kuthamini ubora wa nyumba za Vodacom alitoa wito kwa wananchi ambao tayari wameshafanya malipo ya awali katika nyumba za Iyumbu, kukamilisha malipo yao ili waweze kukabidhiwa nyumba zao ifikapo Oktoba 2022.

"Kwa sasa mradi umefikia asilimia 95 na tunatarajia mradi huu kukamilika kwa silimia 100, ifikapo oktoba 2022, aidha nitoe wito kwa Watanzania wengine wenye furaha na faraja kununua nyumba za kisasa za shirika lao eneo la Iyumbu, kufanya hivyo kwani zimebaki chache’’ alisisitiza Saguya

Katika hatua nyingine, mshindi wa zawadi ya nyumba ya Droo ya Vodacom ya Mpesa imetiki, bi Rahabu Jackson, mkazi wa Manyoni, Singida, alitoa maoni na mtazamo wake kuhusiana na nyumba hiyo iliyojengwa na shirika la nyumba la Taifa (NHC).

"Kwa muda mfupi tu nilioingia ndani ya nyumba na kuikagua, kwakweli ni nyumba siyo nzuri tu bali yenye ubora, na kwa muktadha huo, nawaomba NHC, waendelee kufanya kazi kama hii kwingineko wanakoendelea na miradi ama katika miradi mipya,’’ alisisitiza mshindi huyo wa nyumba, Bi Rahabu Jackson.

No comments:

Post a Comment