Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 6 September 2022

HALMASHAURI ZA MKOA WA TANGA KUNUFAIKA NA MPANGO WA VODACOM M-MAMA


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omari Mgumba amezitaka Halmashauri za mkoa huo kuhakikisha wanajumuisha kwenye mipango ya bajeti na fedha ili kusaidia gharama za usafiri wa dharura kwa kinamama wajawazito pamoja na watoto wachanga wanaohitaji huduma za dharura kwenye vituo vikubwa vya kutolea huduma za afya.

Agizo hilo amelitoa jijini Tanga wakati akizindua mpango wa kuimarisha usafiri wa dharura kwa kinamama Wajawazito na watoto wachanga katika mkoa wa Tanga uliofadhiliwa na Vodacom Tanzania Foundation wakishirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine ikiwamo Touch Foundation na Pathfinder International kuhakikisha wanazuia vifo vya kinamama wajawazito na watoto kwa kuimarisha mfumo wa rufaa pamoja na usafiri wa dharura vijijini kupitia mfumo wa m-mama.

Ambapo amesema mfumo huo umeletwa kwa ajili ya kuondoa na kutatua matatizo ikiwemo ya ucheleweshwaji wa huduma ya dharura ya afya kwa Mama na mtoto mchanga kitu ambacho kinachangia kinamama wajawazito wengi wanapoteza maisha kwa sababu ya Jamii husika kushindwa kufanya maamuzi ya haraka wakati wanajadiliana mama anapoteza maisha hii ikichangiwa na ukosefu wa vyombo vya usafiri wa dharura wa kumtoa nyumbani kumpeleka kituo cha Afya kilicho karibu au hospitali ya wilaya ama ya rufaa.

Hata hivyo alisema mkoa wa Tanga sasa una magari 10 ya kubebea wagonjwa yanayofanya kazi ya kutoa huduma za dharura kwa wagonjwa kwenye vituo vya afya.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa m-mama kutoka taasisi washirika ya Vodafone Foundation, Dolorosa Duncan amesema mpango huo ni suluhisho la kiteknolojia katika kuimarisha rufaa na usafiri wa dharura kwa akina Mama wajawazito na wenye watoto wachanga.

Amesema kupitia mpango huo Vodacom inaunga mkono jitihada za Serikali katika kuzuia vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga kwa kuhakikisha wanaimarisha mfumo wa rufaa pamoja na usafiri wa dharura vijijini ili kuwaepusha na changamoto hizo.

Aidha amesema kwa jinsi wanavyofanya kazi wametengeneza mfumo huo wa m-mama ambao ni wa Serikali kwa asilimia 100 ambapo walianza mwaka 2013 na walitekeleza mfumo huo kwa wilaya mbili za Sengerema na Shinyanga na baadae ukawa katika mkoa wa Shinyanga.

Hatua hivyo alisema baada ya Serikali kujiridhisha kwamba mfumo huo unafanya kazi vizuri sasa wanakwenda nchi nzima na Rais Samia Suluhu Hassan aliuzindua rasmi mnamo Aprili 6 mwaka huu na baada ya hapo Vodacom ikaongeza fedha za ufadhili kutoka Dola za kimarekani milioni 9 walizotoa mwanzo dola milioni 15 ili kuhakikisha mfumo huo unatekelezwa nchi nzima kwa maana ya bara na visiwani.

Alimalizia kwa kusema watakaoupokea mfumo huo wahakikishe wanafanya kazi iliyokusudiwa ya kuokoa maisha ya Mama na Mtoto kwa kuhakikisha usafirishaji wa kukutumia magari ya wagonjwa (Ambulance) na yale yanayotumiwa kutoka kwa jamii yanafanya kazi vizuri kwa kuwalipa madereva kwa wakati ili kufanikisha mradi huo unafanikiwa na hivyo kuokoa maisha ya kinamama na watoto wachanga.

No comments:

Post a Comment