Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 30 September 2022

AZANIA GROUP YAZINDUA UNGA WA NGANO KWA AJILI YA MATUMIZI YA CHAKULA ILI KUONGEZA THAMANI, KULETA SULUHISHO, UTOFAUTI NA KURAHISISHA HUDUMA KWA WATUMIAJI WAKE



29 Septemba 2022 - Azania Group, moja ya chapa kubwa na maarufu ya bidhaa za chakula, imezindua unga mpya wenye thamani na ubora wa hali ya juu na wenye ushawishi kwa watumiaji wake kutumia unga mweupe, laini na wenye kudumu kwa matumizi ya muda mrefu na kukidhi aina mbalimbali za mapishi. Azania Group imezindua chapa yake mpya ya unga iliyopewa jina la AZANIA - PREMIUM HOME FOUR (PHF), Unga wa Ngano ambao sio tu safi lakini pia una ubora wa kimataifa ambao utakidhi mahitaji ya watumiaji. Sherehe ya uzinduzi wa bidhaa hiyo imefanyika Alhamisi 29 Septemba 2022 katika maeneo ya Hellenic Greek Club, Dar es Salaam.


"Unga wetu mpya wa Azania PHF unakuja kama sehemu ya utafiti uliofanywa na kugundua uhitaji wake hivyo ili kuleta suluhu na kuleta utofauti kwenye soko na urahisi kwa watumiaji, Azania tumeonelea vyema kuja na bidhaa hii kwani mara nyingi watu wengi wanabanwa sana na muda na kushindwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kama vile Maandazi, Chapati na vitafunio vingi zaidi na vya aina mbalimbali hivyo bidhaa yetu hii itatoa nafasi ya kuzalisha vitafunio vingi zaidi kuliko vile vilivyozoeleka. ” Alisema Bw Joel Laiser Mkurugenzi wa Biashara wa Azania Group.

 

Akiongeza Bw Joel Laiser amesema “Mvuto wa chakula chochote kile unatokana na muonekano wake na ladha ya chakula husika, hivyo lengo letu katika uzinduzi wa bidhaa hii ni kuongeza faida na kuongeza thamani kwa wateja wetu kwani tunaamini soko letu liko tayari kusambaza bidhaa hii bora kabisa ambayo watumiaji wake watagundua kuwa imetengenezwa kwa ubora na imewekwa viungo vyenye ladha ya hali ya juu."


Wakati wa uzinduzi mmoja kati ya Mama Lishe Maria Mbago ambaye amehudhuria ameeleza kuwa "Nimefurahia kwa mara ya kwanza kutumia bidhaa mpya ya Unga wa Azania PHF ambao ni mweupe na laini kuliko unga mwingine niliotumia hapo awali na la muhimu na kubwa zaidi, unanipa nafasi mimi mpishi kupika haraka zaidi maana ni laini sana na unatoa vitafunio laini na vitamu na vyenye ladha natarajia kuwa bidhaa hii mpya ya Unga wa ngano itanisaidia zaidi kuongeza wateja kutokana na ubora utakaotokana na vitafunwa nitakavyotengeneza kupitia unga huu".

Uzinduzi huo ulipambwa na uwepo wa Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo ambaye amepongeza juhudi za Azania Group katika soko la uzalishaji bidhaa za chakula

“Nimefurahi kujumuika na Azania Group katika tukio hili adhimu na niwapongeze kwa kazi kubwa na mchango mkubwa wanaoutoa katika upatikanaji wa bidhaa za chakula na , uthibitisho wake ni baada ya ujio wa bidhaa yao mpya ya Unga wa Ngano kwa ajili ya kupikia vitu mbalimbali kama vitafunwa na kurahisisha huduma na kazi za upishi kwa watumiaji mbalimbali hususani kwa mama zangu ambao ni Mama lishe lakini pia wanufaika(walaji) wengine na kipekee kabisa naomba niwashukuru kwa kuajiri idadi kubwa ya wafanyakazi kutoka katika wilaya yetu ya Temeke, Lakini pia Azania naomba msiishie kwenye ngano tu, endeleeni kusambaza bidhaa mbalimbali na kuhudumia akina mama ambao ndio wanufaika wakubwa, lakini pia kama vile tunavyofahamu mna bidhaa nyingi zaidi kama vile mafuta ya kupikia, bidhaa ya nazi na nyingine nyingi, tunatumai pia tutaziboresha ili kumletea urahisi Mama Lishe, wanawake na wanaume katika upatikanaji wa chakula bora na chenye manufaa kwa wanaTemeke na Tanzania kwa Ujumla.

Azania Group, imehitimisha kwa kusema “Unga wa Azania PHF utapatikana katika maduka yote Tanzania na yaliyopo mipakani, Sisi kama Azania group tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutoa bidhaa bora, zenye suluhu za huduma kwa watumiaji wetu”

Uzinduzi huo umemalizika kwa wageni waalikwa wote kujivinjari kwa vitafunwa tofauti vilivyotengenezwa na Mama lishe kwa kutumia Unga mpya wa Azania PHF.

KUHUSU AZANIA GROUP

Azania Group, imeundwa chini ya mwamvuli wa makampuni 7, ni mojawapo ya kampuni yenye nguvu na zinazoongoza kiuchumi na imebadilisha maisha ya maelfu ya watu

nchini Tanzania na nje ya mipaka yake, kupitia ushirikishwaji wa biashara pamoja na ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Azania Group ilianza karibu miaka 27 iliyopita, kama biashara ndogo ya familia iliyoanzishwa na Bw. Fuad Edha, Azania imekua polepole kwa miaka mingi, ni dhahiri kwamba katika miaka ya hivi karibuni, Azania Group imekuwa moja ya wazalishaji wakubwa na wasambazaji wa bidhaa zake za chakula muhimu na za nyumbani zinazotengenezwa hapa nchini.

Kundi hili kwa sasa linaendesha viwanda 8 ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na makao yake makuu yapo katika mji mkuu wa biashara wa Dar Es Salaam, Tanzania. Kundi hili lina shughuli zake kote Tanzania, Uganda, DRC Kongo, Malawi, Burundi, Rwanda na Zambia. Mipango iko tayari kueneza biashara zake kwa nchi nyingine kama Afrika Kusini na Nchi zilizopo chini ya Jangwa la Sahara.

Kwa Mawasiliano Zaidi;

Bw Joel Laiser
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Azania Group
0766 076 666

No comments:

Post a Comment