Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 18 August 2022

TAARIFA YA MAUZO YA NYUMBA ZA MEDELI JIJINI DODOMA

  1. Katika muendelezo wa kuwezesha Watanzania wengi zaidi kumiliki nyumba za makazi, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatangaza rasmi mauzo ya nyumba zilizopo eneo la Medeli Jijini Dodoma. Nyumba hizo zipo ndani ya majengo ya ghorofa ya kisasa na zimekamilika zikiwa na huduma zote muhimu za maji, umeme, maeneo ya michezo na maegesho ya magari. Sifa za ziada za nyumba hizo ni kuwa na eneo maalum la kukusanyia taka.
  2. Nyumba zipo katika eneo tulivu la Medeli Jijini Dodoma takriban kilomita moja kutoka katikati ya Jiji na karibu kabisa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uwanja wa Ndege, Stesheni ya Reli na huduma mbalimbali za kijamii. Nyumba zipo chache za kuuzwa kwenye majengo matatu ya ghorofa 4. Usalama katika nyumba hizo umezingatiwa kwa wakazi na wanunuzi kwa kuweka uzio mkubwa.
  3. Kila nyumba ina vyumba vitatu vya kulala, kimoja kati ya hivyo kinajitegemea, sebule iliyoungana na eneo la kula chakula, choo cha umma na jiko kubwa la kisasa. Nyumba hizo zina ukubwa wa mita za mraba 116. 
  4. Kila nyumba itauzwa kwa bei ya TZS 199,870,670. Tunawahamasisha na kuwakaribisha Watanzania wote walio nchini na wanaoishi nje ya nchi wafanye mawasiliano na Ofisi zetu za Makao Makuu ya Shirika, Ofisi za Mikoa au kupitia baruapepe na kukamilisha taratibu mapema kwa ajili ya kuweza kununua nyumba.
  5. Mauzo haya ya nyumba hizi ni mwendelezo wa mauzo ya nyumba za miradi ya NHC yanayolenga kutimiza malengo ya Mpango Mkakati wa Shirika wa miaka kumi (2015/16 – 2024/25).
  6. Ukiwa mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayehitaji kununua nyumba hizo, tafadhali wasiliana na Kitengo cha mauzo kwa Simu Namba 0736 114433; baruapepe: sales@nhc.co.tz au tembelea tovuti ya Shirika www.nhc.co.tz kwa maelezo zaidi.
IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO,
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA.

No comments:

Post a Comment