- Yatoa punguzo la asilimia 10 kwa wateja wanaolipa kwa huduma ya lipa kwa simu pindi wanunuapo simu janja
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mkuu wa Mauzo wa kanda ya Dar es salaam na Pwani, Brigitta Shirima alisema, "Mwaka huu Vodacom tumekuja kivingine ambapo tunatoa wigo mpana wa huduma mbalimbali kwenye maonesho haya ili kuwapa wateja wetu na watanzania kwa ujumla waweze kufurahia huduma zetu, tuna huduma ya 4G ya kweli na punguzo kubwa la asilimia 10 % kama mteja atanunua simujanja kwa njia ya lipa kwa simu.
Tuna huduma kwa jamii kupitia asasi yetu ya Vodacom Tanzania Foundation ambapo tutatoa taarifa kuhusu huduma yetu ya m-mama inayowagusa kinamama kwa kuwapa usafiri pindi wanapopata dharura wakati wa kujifungua, pia tuna huduma ya E-Fahamu ambayo inatoa elimu kwa wanafunzi kwa njia ya kidijitali bila gharama yeyote.”
Aliendelea kusema, kampuni hiyo itatoa huduma ya M-Pesa inayowezesha kufanya huduma mbalimbali za fedha kidijitali kwa simu, VodaBima inayowezesha kupata huduma mbalimbali za bima ya magari na afya, pia wateja wetu watapata huduma ya Paisha App inayowezesha kupata mahitaji mbalimbali mtandaoni.
Pia Brigitta alisema, Vodacom imekuja na bahati nasibu ya Tusua mapene ambapo mteja anatakiwa kutuma neno V kwenda namba 15544 na anaweza kujishindia gari mpya aina ya Suzuki S Presso na pia kuna shindano la Tikisa litakalowezesha wateja wao kujishindia Smart Tv au shilingi milioni 1.
“Mwisho tunahuduma ya M-Kulima inayotoa taarifa mbalimbali za kilimo kidijitali kote nchini, hii itawezesha wakulima kujua pembejeo, bei za mazao, kulipa na kupokea pesa kwa M-Pesa”.
No comments:
Post a Comment