
Mwenyekiti wa bodi ya Tanzania Commercial Bank Dkt. Edmund Mndolwa (katikati), akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kupata faida ya shilingi bilioni 19.7 iliyopata benki hiyo. Wa pilikulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi pamoja na maafisa wengine wa benki hiyo.
Mwenyekiti wabodi ya Tanzania Commercial Bank Dkt. Edmund Mndolwa ametoa taarifa hiyo katika mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar esSalaam na kusema kuwa faida hiyo ni kabla ya kodi.
Faida iliyopatikana mwaka 2021 inatajwa na uongozi wa benki kuwa ni kubwa kufuatia ile ya mwaka 2020 ambayo haijawahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa Benki ya TCB takriban miaka 95 iliyopita.
Amepongeza uongozi pamoja na wafanyakazi wa Tanzania Commercial Bank kwa kuchangia mafanikio hayo licha ya changamoto za mdororo wa uchumi uliosababishwa na wimbi la ugonjwa wa UVOKO-19 ambao pia umeathiri uchumi wa mataifa mengi duniani.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi amesema kufuatia mafanikio hayo, wanahisa wamekubaliana kutoa gawio la hisa na kuelekeza kwenye kuimarisha mtaji wa Benki hiyo.
Mafanikio hayo pia wamewezesha amana za wateja kuongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 1.18 mwaka 2021 kutoka shilingi trilioni 1.04 huku mikopo nayo ikiongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 718.6 kutoka bilioni 617.81
Tanzania Commercial Bank imekuwa ikifanya kazi na wafanyabiashara kuanzia mfanyabiashara mdogo, wa kati na mkubwa na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma kutoka benki ya TCB kila kona ya Tanzania na mipaka yake.
No comments:
Post a Comment