Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 29 June 2022

BENKI YA NBC KUBORESHA MALIPO NA MAKUSANYO YA SERIKALI ZANZAIBAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), na Mkurugenzi wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar, Said Seif Said, wakikabidhiana Mikataba ya Maridhiano baada ya Benki ya NBC kuingia makubaliano na taasisi hiyo kwa ajili ya kuweka mfumo wa ukusanyaji wa mapato na malipo ya Serikali ya Zanzibar. Hafla hiyo fupi ya utiaji saini ilifanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Airport.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili Kulia) na Mkurugenzi wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar, Said Seif Said (wa pili kushoto) wakionyesha Mikataba ya Maridhiano iliyoigiwa baina ya Benki hiyo na Taasisi ya e-GAZ kwa ajili ya kuweka mfumo wa ukusanyaji wa mapato na malipo ya serikali ya Zanzibar. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa NBC, James Meitaron na Haja Lissa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mifumo na Miundombinu ya TEHAMA Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili Kulia) na Mkurugenzi wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar, Said Seif Said (wa pili kushoto) wakionyesha Mikataba ya Maridhiano iliyoigiwa baina ya Benki hiyo na Taasisi ya e-GAZ kwa ajili ya kuweka mfumo wa ukusanyaji mapato na malipo ya serikali ya Zanzibar.

Jumanne, Juni 28, 2022 - Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesaini Mkataba wa Maradhiano na Wakala wa Serikali Mtandao (e-government) Zanzibar, kwa ajili ya kuweka mfumo wa ukusanyaji mapato na malipo ya serikali ya Zanzibar. 

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba huo jijini Zanzibar, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema; “Benki ya NBC inaendelea kuwekeza katika mifumo ya TEHAMA ili kutoa masuluhisho ya kibenki kwa makundi yote ya wateja. Leo tunajivunia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Zanzibar chini ya ya Rais Hussein Mwinyi, katika kuiboresha sekta ya fedha kwa kuingiza mifumo ya kidigitali ili kuongeza ufanisi hususan katika kuboresha makusanyo ya mapato ya serikali na malipo kwa wadau wake” alisema. 

Ushirikiano huu utaiwezesha serikali ya Zanzibar kukusanya mapato kwa wakati na kwa kuwapa wateja urahisi wa kufanya malipo ya Serikali kwa urahisi katika matawi ya Benki ya NBC, Mawakala, au kupitia huduma kwa njia ya mtandao kupitia simu za mkononi na kwa njia ya mtandao wa intaneti. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa e-GAZ, Said Seif, alisema, “Tunafuraha kushirikiana na Benki ya NBC, moja ya Benki kubwa nchini Tanzania, katika kuweka mfumo wa kidigitali wa makusanyo na malipo ya Serikali hapa Zanzibar. Kama wakala uliopewa dhamana ya uwekaji mifumo ya digitali Zanzibar, tuna dhamira ya kuhakikisha kuwa tunashirikiana na wadau wote wenye uwezo katika kufikia kiwango cha juu kidijitali katika taasisi za umma hapa Zanzibar” alisema.

No comments:

Post a Comment