Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday 24 April 2022

STANDARD CHARTERED KUTOA FEDHA ZAIDI UJENZI WA SGR

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kushoto), na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango- Zanzibar Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya Standard Chartered, baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Standard Chartered Tanzania Bw. Sanjay Raghani, Katibu Mkuu, Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil, Mwenyekiti wa Standard Chertered, Bw. Jose Vinals.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) (wa tano kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya Standard Chartered Pamoja na Ujumbe wa Tanzania, baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa Benki ya Standard Chartered duniani Bw. Jose Vinals, baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), na Mwenyekiti wa Benki ya Standard Chartered Bw. Jose Vinals, wakibadilishana kadi za mawasiliano baada ya kumalizika kwa mkutano wao kuhusu uwekezaji kwenye miradi ya kimkakati nchini Tanzania, uliofanyika Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb), akisalimiana na Mwenyekiti wa Benki ya Standard Chartered Bw. Jose Vinals, baada ya kumalizika kwa majadiliano kati ya Ujumbe wa Tanzania na Benki hiyo kuhusu upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miradi uliofanyika Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango- Zanzibar Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Standard Chertered Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, baada ya kumalizika kwa majadiliano kati ya Ujumbe wa Tanzania na Benki hiyo kuhusu upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo, uliofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati wa kikao kati ya ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa Benki ya Standard Chartered kuhusu upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati nchini Tanzania. Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Washington DC, Marekani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Benki hiyo duniani Bw. Jose Vinals.

Benny Mwaipaja, Washington DC

Benki ya Standard Chartered imeihakikishia Tanzania kuwa iko tayari kutoa fedha zaidi kwenye miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ikiwemo Reli ya kisasa ya SGR na ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege.

Ahadi hiyo imetolewa na Uongozi wa Benki hiyo ukjongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Jose Vinals, ulipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Tanzania, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb). kando ya mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini Washington DC, Marekani.

Akizungumza baada ya kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Washington DC, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba alisema kuwa Benki hiyo ilitoa mkopo unaotumika kujenga reli ya kisasa ya SGR kutoka Morogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, na kwamba hivi sasa Serikali iko kwenye mazungumzo na Benki hiyo ili itoe mkopo mwingine kwa ajili ya vipande vingine vya reli hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Mheshimiwa Saada Mkuya Salum, alisema kuwa katika kuimarisha shughuli za utalii na kukuza uchumi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepanga kuboresha miundombinu ya Uwanja wa Ndege wa Pemba na kwamba mazungumzo yanayoendelea kati ya Serikali na Benki hiyo yatawezesha kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Standard Chartered baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki hiyo nchini Tanzania Bw. Sanjay Rughani, alisema kuwa wako tayari kutoa fedha zaidi kwa ajili ya miradi iliyowasilishwa na Serikali kwenye Benki hiyo.

Alisema kuwa pamoja na ahadi ya kutoa fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali, Benki hiyo pia iko tayari kuwashawishi wawekezaji wengine kutoka maeneo mbalimbali duniani kwenda kuwekeza mitaji na teknolojia nchini Tanzania.

Ikumbukwe kwamba Benki ya Standard Chartered, tarehe 13 Februari, 2020, iliipatia Tanzania mkopo wenye thamani ya dola za Marekani, bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha kuanzia Morogoro hadi Makutupora, mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment