Wafanyakazi wa SBL Moshi kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi mablanketi 150 kwa Mwika Rotary Club kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo kata ya Mwika mkoani Kilimanjaro. |
Aprili 9, 2022 - Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetoa msaada wa mablanketi 150 kwa wazee Mwika mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wake wa kuisaidia jamii. Msaada huo kwa wazee ulipokabidhiwa kwa niaba yao kwenda kwa Mwika Rotary Club.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa kiwanda cha SBL Moshi, Alice Kilembe alisema kampuni hiyo inajivunia kutoa ushirikiano kwa Mwika Rotary katika kuwathamini na kuwahudumia wazee wanaoishi katika eneo hilo.
‘Mchango tunaoutoa leo kwa wazee ni ishara ya upendo na shukrani zetu kwa kazi nzuri waliyoifanyia taifa letu katika enzi za ujana wao." Jamii inapaswa kutunza kikundi hiki, na SBL inajivunia kuwa sehemu hii. Tunaamini mablanketi yatawalinda na baridi kali msimu utakapofika,' alisema.
Sambamba na mchango huo kwa Mwika Rotary Club, Alice alisema kuwa SBL imekuwa ikitekeleza programu kadhaa za kusaidia jamii ambazo hadi sasa zimenufaisha mamilioni ya watu nchini kote.
"Mnamo mwaka 2019, SBL tulianzisha mpango wa ufadhili wa masomo kwa ajili ya wanafunzi wanaosomea masomo ya kilimo katika vyuo vya ndani ili kuunga mkono jitihada za serikali za kupanua wigo wa wataalamu wa kilimo nchini, na hadi sasa zaidi ya 200 wamenufaika na mpango huu," alitolea mfano.
"Aidha tumejipanga na tunaendelea na programu nyingi za kusaidia jamii, kama vile kuhakikisha waishio vijijini wanapata maji safi na salama (programu maarufu ijulikanayo kama Water of Life). Hadi sasa tumetekeleza miradi 22 ya maji katika maeneo mbalimbali nchini tangu mwaka 2010, ambapo watu zaidi ya watu milioni mbili wamenufaika’, alikiri.
Programu nyingine alizozitaja meneja huyo wa kiwanda ni pamoja na kilimo biashara, ambacho huwasaidia wakulima wakubwa na wadogo kuongeza uzalishaji huku wakiwaandalia mazingira ya masoko kwa ajili ya mavuno yao.
Aliyekuwa Rais wa Mwika Rotary Club, Ester Towo, ambaye alimwakilisha rais wa sasa, Godrick Lyimo, aliishukuru SBL kwa msaada huo, akibainisha kuwa mchango huo ni chachu kubwa kwa shirika hilo, ambalo linategemea michango hiyo ili kuendelea kuihudumia jamii ya Mwika.
"Tunafurahishwa sana na mchango wa blanketi 150 kutoka kwa SBL kusaidia wazee wa Mwika na maeneo ya jirani hasa wakati huu wa mwaka ambapo baridi linakaribia. Mablanketi haya yatawawezesha wazee kupata joto la kutosha wakati wa msimu wa baridi kali hapa Mwika," anasema.
‘Wazee wengi wanaoishi majumbani mwao wanakosa msaada kwa sababu hawana mtu wa kuwahudumia. Hivyo basi, mchango huu ni mkubwa sana kwao ambao utawafanya wahisi kuthaminiwa na kutambuliwa kwa mara nyingine. Ahsante, SBL,' alimalizia.
About SBL:
Incorporated in 1988 as Associated Breweries, SBL is the second largest beer company in Tanzania, with its beer brands accounting for over 25% of the market by volume.
SBL has three operating plants in Dar es Salaam, Mwanza and Moshi.
Since the creation of SBL in 2002, the business has grown its portfolio of brands year on year. The majority stake acquisition by EABL/Diageo in 2010 has seen increased investment in international quality standards leading to greater job opportunities for the people of Tanzania.
SBL Brands have been receiving multiple international awards and include Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Pilsner King, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout and Senator. The company is also home to world’s renowned spirits such as Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum and Baileys Irish Cream.
For further information contact;
John Wanyancha
SBL Corporate Relations Director
Tel: 0692148857
Email: john.wanyancha@diageo.com
No comments:
Post a Comment