Kuna vifurushi viwili kwenye bima hii;
Bima ndogo (J-Afya) ambayo inamkinga mteja kwa ajili ya matibabu ya kutwa na kulazwa. Katika kifurushi hiki, Bima itagharamia mwanachama na familia yake kwa mwaka, Sh. Milioni 6 kwa matibabu ya kulazwa, na Milioni 1.2 ya kutwa.
Mtoto pekee yake atagharamiwa kwa Sh. Milioni 3. Kutakuwa na gharama za ziada endapo mwanachama atahitaji huduma zaidi ya zilizoainishwa kwenye mpango wake wa bima.
Aidha, Bima kubwa (J-care) imegawanyika katika makundi manne; Royal, Executive, Advanced na Premier, na malipo ya kila mwaka (Premium) yatategemea na ukubwa wa familia pamoja na umri wa mwanachama na mwenza wake.
Faida ya bima hii ni kupata matibabu ya kutwa na kulazwa, matibabu ya meno na macho, mkono wa pole endapo mwanachama atafariki, uzazi na vipimo vikubwa kama MRI.
Bima ya J-care inakupa huduma bora za matibabu kwa urahisi katika hospitali zilizoko kwenye mpango wa bima zinazopatikana nchi nzima.
Pata bima yako kupitia *150*68# au kupiga simu nambari 0800 002 002 bure Kabisa, barua pepe Bancassurance@nmbbank.co.tz au fika tawi la NMB lililopo karibu yako.
Umebima?- SiNgumuKihivyo!
No comments:
Post a Comment