Sehemu ya Vitanda vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Hospitali ya Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora. |
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkundutsi iliyopo Kasulu, Kigoma wakiwa wamekalia viti na kutumia meza zilizotolewa kwa shule hiyo na Benki ya NMB. |
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uhuru ya Shinyanga mjini wakiwa wamekalia viti na kutumia meza zilizotolewa kwa shule hiyo na Benki ya NMB kama msaada kupunguza uhaba wa vifaa hivyo. |
Kwa namna ya kipekee, benki hii imekuwa ikishiriki katika masuala mbalimbali hususani katika sekta ya afya na elimu.
Kama ilivyo katika mikoa mingine yote nchini, mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga imekuwa wanufaika wakubwa wa namna benki hii inavyowajibika kwa jamii.
Ziara maalum ya watumishi wa Benki ya NMB katika mikoa hii wameshuhudia wanufaika wa misaada hiyo wakieleza namna ambavyo mchango wa NMB katika taasisi zao umekuwa chachu ya hatua kubwa sana za kimaendeleo kwao na jamii kwa ujumla.
Kwa mwaka 2021 mikoa hii ya Tabora, Shinyanga na Kigoma, jumla ya shule 23 zilipata madawati na kusaidia katika kuwatengenezea mazingira mazuri ya kusomea kwa wanafunzi. Hii imekuwa chachu ya ufaulu na kupunguza utoro kwa wanafunzi kwani wengi wao sasa hukaa katika madawati na madarasa yalioezekwa.
Vilevile, taasisi 12 zilipata vifaa vya kuezeka huku vituo vya afya vinne vikipata vifaa tiba vinavyosaidia na kurahisisha utoaji wa huduma za afya kwa wakazi wa maeneo hayo.
Vifaa vya hospitali vilivyotolewa katika hospitali na vituo vya afya mbalimbali katika mikoa hiyo, vimekuwa chachu ya kuongeza idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa kwa ufasaha pamoja na kupunguza changamoto walizokuwa wanakumbana nazo. Suala la wagonjwa kulala wawili wawili katika vitanda linamalizwa na vitanda vinayotolewa na taasisi hii ya fedha kubwa zaidi nchini.
Mashuka, vitanda vya kujifungulia, vifaa vya kuezeka ni vitu vingine pia ambavyo benki ya NMB imekuwa ikitoa kwa Hospitali na vituo vya afya katika mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga. Hospitali za wilaya na hata zahanati zimekuwa wanufaika wakubwa sana wa uwajibikaji huu wa NMB kwa jamii.
No comments:
Post a Comment