Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Foreign Exchange Rates
Selcom Pesa Advert_110225
Standard Chartered Advert_300125
DStv Advert_090724
Tuesday, 25 January 2022
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZINDUA TAWI JIPYA KATAVI
Tanzania Commercial Bank (TCB) imezindua tawi jipya Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mpanda ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma za kibenki kwa wateja na Wananchi kwa ujumla.
Tawi hilo la kwanza kwa taasisi za fedha kuzinduliwa Mkoa Katavi Wilaya ya Mpanda, limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko .
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Sabasaba Moshingi alisema huo ni mwendelezo wa Tanzania Commercial Bank katika kusogeza huduma kwa wateja wake.
Alisema tawi hilo jipya la Mpanda litarahisisha utoaji huduma za kibenki kwa wateja wake hali ambayo itapunguza mzunguko wa wananchi kuzifuata huduma za kibenki maeneo mengine ya mbali.
Aliongeza kuwa Tanzania Commercial Bank (TCB) imezingatia shughuli za kiuchumi zinazoendeshwa Wilayani humo kwa wafanyabiashara, wafugaji na wakulima na kufungua tawi hilo hivyo wateja hawatalazimika kwenda mjini kupata huduma za kibenki kama hapo awali.
Alisema Tanzania Commercial Bank sio kwamba tu ni benki kubwa nchini, bali inatoa mchango mkubwa katika shughuli za kijamii hasa kuinua elimu pamoja na Afya.
Kwa kuona umuhimu wa kusongeza huduma kwa wateja hasa maeneo ya vijijini Tanzania Commercial Bank (TCB) inaendelea kuwawezesha mawakala watakaosaidia kutoa huduma hizo jambo ambalo litasaidia kusogeza huduma kwa wateja wetu nchi mzima.
Aliongeza, kwa sasa Benki hiyo ina matawi 82, mawakala tunao zaidi 3,800, mashine zakutolea pesa ATM zetu tunazojitegemea Kama Tanzania Commercial Bank ni 84 lakini zile ATM ambazo tupo chini ya Umoja Switch ni zaidi ya 250.
Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko ameupongeza uongozi wa Tanzania Commercial Bank kwa kuja kuwekeza katika Mkoa huu na anaamini kwa wingi wa watu waliojitikeza katika tukio hili watakwenda kufungua akaunti.
Mrindoko pia ameipongeza Tanzania Commercial Bank (TCB) kwa kufika Mkoani Katavi na kuwakaribisha kwani fursa zipo nyingi katika mkoa huo zikiwemo za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara pamoja na mazao mengine ya kimkakati.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliuhakikishia uongozi wa Tanzania Commercial Bank (TCB) kwamba Katavi ni Mkoa unaokua kwa kasi sana kutokana na shughuli za uzalishaji na za kimaendeleo hivyo huduma ya Tanzania Commercial Bank kwakufungua tawi hilo limekuja wakati muafaka
“Kuzinduliwa kwa Tawi la Tanzania Commercial Bank (TCB) hapa Katavi maana yake ni kwamba huduma za kibenki zitapatikana kwa urahisi zaidi hivyo wafanyakazi, wakulima na wafanyabiashara wa Katavi changamkieni fursa hii na kuja kufungua akaunti na kufanya miamala mengine kama kulipa kodi za serikali.” alisisitiza Mrindoko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment