Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 6 January 2022

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI KUENDELEA KUSAIDIA MAENDELEO YA KIJAMII NA KIUCHUMI

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia mradi wa kusaidia baa kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19 maarufu kama Raise the Bar inatoa vifaa mbali mbali vinavyosaidia kuboresha usafi wa mazingira ya baa na hivyo kulinda afya za wateja. Kupitia mradi huu SBL imtenga zaidi ya shilingi bilioni 2.

Wakati taifa likiuaga mwaka 2021 na kuukaribisha mwaka 2022, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imesema itaendelea na jitihada zake za kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye nyanja mbali mbali ikiwamo kilimo, mazingira, elimu pamoja na michezo.

Mwendelezo wa hatua hii ya SBL unakuja wakati Serikali ikitilia mkazo suala la ushirikiano kati ya sekta binafsi ya umma katika kuwaletea wananchi maendeleo katika sehemu mbali mbali hapa nchini.

Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL wa John Wanyancha alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kyusidia jamii na kuongeza kuwa itaendeleza jitihida hizo ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono Serikali katika kuboesha maisha ya watanzania.

Kupitia mpango wetu wa kusaidia jamii tunazo programu mbali mbali mbali ambazo zimegusa maisha ya watu kwa namna tofauti. Programu hizo ni pamoja na Maji ni Uhai, Kilimo Viwanda, Kilimo Biashara pamoja na Unywaji wa Kistarabu,’ alifafanua mkurugenzi huyo.

Akizungumzia kuhusu programu ya ‘Maji ni Uhai’ alisema SBL imesaidia uchimbaji wa visima vilivyosaidia upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbali mbali ikiwamo Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwezesha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa zaidi ya watu milioni moja.

“Pia katika programu yetu ya kusaidia kuongeza idadi ya wataalamu wa kilimo hapa nchini kupitia ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaosomea kilimo tumeweza kutoa ufadhili kwa wanafunzi 71 ambao wataongeza nguvu katika sekta ya kilimo ambayo ndiyo uti wa mgongo kwa uchumi wa nchi yetu,’ alifafanua

Wanyancha alitaja programu nyingine kuwa ni Kilimo Biashara ambapo SBL inafanya kazi na mtandao wa wakulima zaidi ya 400 hapa nchini ambao huwasaidi kwa kuwapa mgegu bora bure Pamoja na wataalumu wa kilimo huku ikiwahakikisha soko la mazao yao ambayo ni shayiri, mahindi na mtama.

Mkurugenzi huyo anasema kupitia programu hiyo, SBL huwaunganisha wakulima na mabenki ambayo huweza kujipatia mikopo na kupanua shughuli zao za kilimo na kuongeza kuwa kampuni hiyo inanunua asilimia 80 ya mahitaji yake ya maligha kwa mwaka ambayo ni tani 17,000 ikiwa na lengo lakufikia tani 25,000 kufikia kwama 2025.

Kupitia elimu juu ya unywaji wa kistarabu anasema kampuni hiyo imeweza kuwafikia zaidi ya watu laki 3 hapa nchini huku ikitoa elimu juu ya madhara ya kunywa na kuendesha vyombo vya moto kupitia kampeni ya “Usinywe,na Kuendesha vyombo vya Moto”“Tumekuwa tukishirikiana na wadau mbali mbali ikiwamo jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani katika kuhamasisha usalama bara barani. Tumekuwa tukiwapa elimu hii maderava wa mabasi, boda boda, waenda kwa miguu,” alisema

No comments:

Post a Comment