Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 17 November 2021

DStv YAFUNGA MWAKA NA ZIGO LA SIKUKUU!

Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo akifafanua kuhusu kampeni ya msimu wa sikukuu ijulikanayo kama ZIGO la Sikukuu ambapo DStv inatoa ofa maalum kwa wateja wake. Kampeni hiyo ZIGO la Sikukuu ilizundiliwa rasmi jana katika Makao Makuu ya Ofisi za MultiChoice Tanzania, Kinondoni Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mheshimiwa Jokate Mwegelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Zigo la Sikukuu. Kampeni hiyo ZIGO la Sikukuu ilizundiliwa rasmi jana katika Makao Makuu ya Ofisi za MultiChoice Tanzania, Kinondoni Dar es Salam.
Wafanyakazi wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania katika picha ya pamoja wakifurahia Kampeni ya ZIGO la Sikukuu jana katika ofisi za Makao Makuu ya MultiChoice Tanzania zilizopo Kinondoni Dar es Salaam, Tanzania.

Dar es Salaam, Novemba 16 2021 - Katika kunogesha zaidi shamrasharma za msimu wa sikukuu, kampuni ya MultiChoice Tanzania imetangaza ofa maalum kwa wateja wapya wa DStv yenye lengo la kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanapata huduma hiyo ili waweze kufurahia burudani elimu na habari wao na familia zao msimu huu wa sikukuu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya DStv iliyopewa jina la ‘ZIGO la Sikukuu, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo amesema kama ilivyo ada kwa DStv, kila unapofika msimu wa sikukuu hutoa ofa maalum kwa wateja wake ili kuwapa uhakika wa kupata huduma za DStv kipindi hiki ambapo ni cha sikukuu na watu wengi wakiwemo watoto huwa likizo hivyo kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa burudani nyumbani.

“Kwa wale ambao bado hawajajiunga na DStv, huu ndio wakati muafaka kwani kuna muendelezo wa ofa maalum ya DStv Poa iliyoanza Septemba mwaka huu ambapo kwa kuwajali wateja wetu tuliona kuwa kuna umuhimu kwa ofa hii kuendelea kuwepo sokoni katika msimu huu wa Sikukuu. Kupitia mwendelezo wa ofa hii maalum mteja ataweza kuunganishwa kwa Shs. 59,000/- na zawadi ya kifurushi kipya cha DStv Poa mwezi mmoja bila malipo. Aliongeza kuwa ofa hii inawapa uhakika wateja wetu wapya kufurahia maudhui motomoto ndani ya DStv na itadumu hadi mwanzoni mwa mwezi Januari 2022.

Sambamba na muendelezo wa ofa hii maalum wateja wetu wa DStv pia wataendelea kupata maudhui kemkem katika ZIGO hili la Sikukuu lililosheheni burudani mbalimbali kuanzia Filamu, Tamthilia mpya za kinyumbani kama Danga na La Familia, bila kusahau filamu za kimataifa, vipindi bora vya Watoto ambao sasa wanaanza likizo ikiwemo cartoon network, Disney, Nickelodeon, CBeebies, Boomerang, JimJam na Davinci zikiwa kwa Lugha ya kingereza wakati chaneli ya Mambo Moto sasa inakuletea vipindi bora vya Watoto vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Na kwa wapenzi wa michezo, Msimu huu wa sikukuu watapata kufurahia mechi zaidi ya 100 ndani ya Premier League, Laliga, Serie A na UEFA champions league na Europa League ndani ya DStv pekee.

Akifafanua zaidi kuhusu ofa hiyo maalum inayopatikana nchi nzima, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema kuwa mawakala wa DStv wanapatikana kote nchini hivyo mteja atapata ofa hii na huduma ya kufungiwa DStv popote alipo kwa urahisi na haraka. “Tunafahamu kuwa kipindi hiki cha sikukuu watu wengi husafiri kuungana na familia zao maeneo mbalimbali mijini na vijijini na kwa kulitambua hili tumejipanga kuhakikisha huduma zetu zinapatikana kirahisi kila mahali”

Amewashauri wateja wote ambao wanahitaji huduma za DStv, mbali na kwenda kwenye vituo au mawakala wa DStv, wanaweza pia kupata huduma hiyo kwa kupiga simu 0659 07 07 07 au kwa kutembelea kurasa za DStv Tanzania za mitandao ya kijamii Instagram @dstvtanzania, Twitter @DStv_Tz na Facebook @DStv(tz) ambapo wanaweza kupata huduma mbalimbali za DStv kama vile kuunganishwa, kulipia vifurushi, kubadili kifurushi na huduma nyinginezo.

Kwa wale wanaosafiri, amewakumbusha kupakua DStv App inayowawezesha kuendelea kufurahia huduma za DStv kwenye vifaa mbalimbali kama simu janja bila gharama yaziada. “kwa wale wanaosafiri na wangehitaji kuendelea kuburudika na DStv, ni vyema wakatumua huduma yetu ya DStv App kwa kupakua app yetu na hivyo kuweza kutumia akaunti zao katika vifaa zaidi ya vine popote walipo nchini bila kulazimika kulipia malipo yoyote ya ziada” alisisitiza Shelukindo

Hafla ya kuzindua kampeni hiyo ya Zigo la Sikukuu ilihudhuriwa na baadhi ya wasanii maarufu wa Bongo Movie wanaoigiza katika tamthilia na filamu mbalimbali zinazoonyeshwa kwenye chaneli ya Maisha Magic Bongo ndani ya DStv wakiwemo waandaji wa tamthilia mpya za Danga na Familia.

Kufahamu zaidi kuhusu maudhui motomoto msimu huu wa sikukuu tembelea https://www.dstvafrica.com/en-tz

No comments:

Post a Comment