Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 20 October 2021

VODACOM YAONGEZA IDADI YA MATUMIZI YA MAWASILIANO, HUKU NCHI IKIPITIA MABADILIKO CHANYA YA KIDIJITALI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom Tanzania Plc, Jaji mstaafu, Thomas Mihayo akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mkutano wa mwaka wa wanahisa wa kampuni hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom Tanzania Plc, Jaji mstaafu, Thomas Mihayo akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mkutano wa mwaka wa wanahisa wa kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo, Jacques Marais na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Vodacom Plc anayemaliza muda wake, Hisham Hendi.
  • Pamoja na mazingira yenye changamoto, dalili chanya za mabadiliko zimeripotiwa
  • Jumla ya Shilingi bilioni 549.3 zimelipwa kama gawio tangu kampuni ilivyoorodheshwa kwenye soko la hisa miaka minne iliyopita
Kampuni inayoongoza ya teknolojia na mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania Plc hivi karibuni imefanya mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa ambapo ripoti ya fedha kwa mwaka unaoishia tarehe 31 Machi 2021 iliwasilishwa. Taarifa hii inaelezea kuhusu biashara kwa ujumla, mfumo wa biashara na mazingira ya kazi ya kampuni ya Vodacom Tanzania na kupitia ufanisi wake katika nyanja za utawala na biashara.

Katika ripoti hiyo, mapato ya Shilingi 966 bilioni yaliripotiwa, ikiwa yameshuka kwa asilimia 5.7 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Viashiria vingine vilivyoripotiwa ni mapato ya Shilingi 356.8 bilioni ikiwa ni mapato ya M-Pesa na Shilingi 186.9 bilioni ikiwa ni mapato yatokanayo na huduma za data, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.3.

Akizungumza kwa mara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kuwa Mwenyekiti ya Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom Tanzania Plc, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aligusia mazingira ya biashara kwa mwaka uliopita na jinsi kampuni ilivyokabiliana nayo ”Jibu la Vodacom kwa mlipuko wa ugonjwa na nguvu iliyoonekana katika ufanisi wake kifedha katika mazingira magumu kwenye maswala ya bei za huduma na shinikizo za kisheria ni ushahidi wa umahiri wa mkakati wake. Katika kutekeleza mkakati huo, kampuni imetimiza malengo kadhaa ili kuhakikisha usalama na ustawi wa wafanyakazi wake na kuendelea kuunganishwa kwa watu binafsi, jamii, biashara na serikali kwa kutunza ubora wa mtandao wake.”

Mwaka wa fedha 2020-2021 ulikuwa na changamoto kwa nchi nzima lakini sekta ya mawasiliano ilikuwa na changamoto zake maalum. Changamoto hizi zilielezwa na Hisham Hendi, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, “Kwa mtazamo wa kifedha, mapato na faida ziliathirika vibaya kutokana na kuzuiwa kwa a kwa kadi za SIM za wateja 2.9 milioni mwishoni mwa mwaka wa kifedha uliopita pamoja na ongezeko kubwa la ushindani. Pia, kudorora kwa shughuli za kiuchumi kutokana na mlipuko wa ugonjwa kulipunguza matumizi ya wateja. Pamoja na sababu hizi kuchangia punguzo la asilimia 5.7 za mapato yatokanayo na huduma, kulikuwa na ongezeko la ukuaji wa mapato katika nusu ya pili ya mwaka, hii ikichagizwa na na ongezeko la mapato ya data na matumizi ya M-Pesa.”

Uhitaji wa huduma za data na M-Pesa bado uko juu, jambo ambalo ndiyo msingi wa mkakati wa kampuni katika swala la ushrikikishwaji kifedha na matumizi ya data. Vodacom inaendelea kuwekeza na kupanua mifumo yake hii na inategemewa kuwa maeneo haya yataendelea kuwa chanzo kikuu cha ukuwaji katika siku za mbele. Vodacom pia imechukuwa hatua Madhubuti kuhakikisha inajenga vyanzo vingine vya mapato kutokana na kuboresha huduma za kidijitali zinazolenga kuwapatia wateja huduma nyingi zaidi kupitia mifumo ya kidijitali.

Akiangalia siku zijazo, Mwenyekiti alisema, “Ili michango ya wafanyabiashara kwa jamii itimie kikamilifu nchini Tanzania, ni muhimu tuendane na serikali na taasisi zinazosimamia sekta yetu ili kujenga mahusiano ya kuaminiana na kuheshimiana. Kuongeza kasi ya kufanya ivyo, tunahitaji kutafuta mbinu za kuboresha majadiliano na kutatua tofauti zinazoweza kutokea kati ya serikali, taasisi za usimamizi na wafanyabiashara.”

Iliripotiwa pia kwa wanahisa kuwa Mkurugenzi Mkuu, Bw. Hisham Hendi ataondoka na kushika nafasi mpya katika kampuni mama ya Vodafone Group nchini Hispania. Mwenyekiti alimtakia kheri akisema, “Kwa niaba ya Bodi, napenda kumshukuru Hisham Hendi ambaye chini ya utawala wake, vodacom iliendelea kuongoza sekta ya mawasiliano nchini kwa kutekeleza mkakati wa kidijitali ambao umeongeza kasi ya ushirikishwaji kifedha kupitia huduma bunifu, na kwa kuwa shinikizo la uwekezaji katika upatikanaji huduma kwa mamilioni ya Watanzania ambao huko nyuma walikuwa hawana uwezo wa kupata huduma za mawasiliano. Namtakia Hisham na familia yake kila la heri katika Maisha yao mapya.”

No comments:

Post a Comment