Mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Jijini Dar es Salaam. |
Tanzania na Ufaransa zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo ya kimkakati ikiwemo Nishati, Elimu, Kilimo na Miundombinu ambapo Ufaransa imekubali kukarabati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘Terminal Two’ Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester hivi karibuni alipowasili Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Kumekuwa na Miradi ambayo Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lao la Maendeleo wamekuwa wakifadhili Miradi mbalimbali katika Sekta mbalimbali hapa nchini zikiwemo sekta za Nishati, Elimu, Kilimo na Miundombinu.
Mtakumbuka kuwa Ufaransa ndiyo waliojenga Uwanja wa Ndege wa “Termirnal Two” wa Julius Kambarage Nyerere sasa wanakuja na mradi wa kukarabati uwanja huo na kuufanya kuwa wa kisasa zaidi. Sasa hivi tu terminal three lakini terminal two imekuwa ikitumika na ndege zinazofanya safari zake za ndani hapa nchini……..mradi huu ni moja kati ya mradi mkubwa na utakamilika hivi karibuni.
Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester yupo nchini Tanzania kuzindua safari za Shirika la ndege la Ufaransa ‘Fance Airline’ kutoka Paris hadi Zanzibar ambapo mara ya mwisho kwa shirika hilo kufanya safari zake hapa nchini ilikuwa mwaka 1974.
Septemba 15, 2021 Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Nabil Hajlaouvi alisema Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la ndege ‘Fance Airline’ inategemea kuanzisha safari mpya ya ndege kutoka Ufaransa moja kwa moja hadi Zanzibar kuanzia 19 Oktoba 2021.
Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Colin Powell.
“Kwa kweli Serikali ya Tanzania tumeshtushwa sana na kifo chake katika kipindi chake aliendeleza uhusiano wa Marekani na Mataifa mbalimbali, kwa kweli ni masikitiko makubwa tutamkumbuka daima,” Amesema Balozi Mulamula.
No comments:
Post a Comment