Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 25 October 2021

BIA YA PILSNER KUDHAMINI MISS KANDA YA ZIWA 2021

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mwanza, Patrick Kisaka, akiwaongoza baadhi ya warembo wanaowania taji la Miss Kanda ya Ziwa 2021 walipofika kutembelea kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo jijini Mwanza. Mashindano hayo yamedhaminiwa na Bia ya Pisner inayozalishwa na kiwanda hicho.
Warembo wanaoshiriki katika shindano la Miss Kanda ya Ziwa wakifuatilia mafunzo ya kuchukua tahadhari dhidi ya Covid-19 kabla ya kuanza kutembelea kiwanda cha Serengeti kilichopo jijini Mwanza. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Bia ya Pilsner inayozalishwa na kiwanda hicho.
Meneja Uzalishaji wa kampuni ya Bia ya Serengeti Mwanza, Rolinda Samson (wa kwanza kulia) akizungumza na warembo wanaoshiriki shindano la Miss Kanda ya Ziwa waliotembelea kiwanda hicho jana. Kulia kwake ni Meneja Mauzo wa SBL, Patrick Kisaka.
Mhandisi wa Uzalishaji katika kiwanda cha Bia ya Serengeti tawi la Mwanza, Isaya John (kulia) akiwapa maelezo warembo wanaoshiriki shindano la Miss Kanda ya Ziwa 2021 juu ya namna bia inavyotengenezwa walipotembelea kiwanda hicho jana.

No comments:

Post a Comment