Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 4 October 2021

BENKI YA DCB YASAIDIA KUFANIKISHA KILELE CHA MAADHIMISHO YA 20 YA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF)

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Doroth Gwajima (kushoto), akikabidhi cheti cha shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya NHIF kimefanyika Jijini Dodoma juzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB Godfrey Ndalahwa akizungumza Jambo na Mkaguzi wa Ndani wa Mfuko wa Bima ya Afya, Grace Temba (kushoto), wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) jijini Dodoma juzi. Benki ya DCB iikuwa ni moja ya taasisi zilizojitokeza kufanikisha maadhimisho hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB Godfrey Ndalahwa (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa NHIF, Celestine Muganga (kushoto) huku Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya DCB, Nelson Swai wakisikiliza wakati walipokwenda kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) yanayofanyika Jijini Dodoma.
Kutoka kulia pichani; Meneja wa Benki ya DCB Tawi la Dodoma, Daniel Buzuka, Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa benki hiyo, Nelson Swai na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa wakihudhuria Kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya NHIF pamoja na washiriki wengine Jijini Dodoma juzi.

No comments:

Post a Comment