Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Saturday, 2 October 2021
BENKI YA BIASHARA YA DCB YAWAPONGEZA VIONGOZI WAKE UTEUZI TANESCO
Dar es Salaam, Septemba 27, 2021 - Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Benki ya Biashara ya DCB imewapongeza viongozi wake wawili Mwenyekiti wa Bodi ya DCB Ndg. Maharage Chande na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Bi Zawadia Nanyaro katika uteuzi uliofanywa na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan na kutangazwa Septemba 25,2021. Mheshimiwa Rais amemteuwa Ndugu Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, na kwa mujibu wa utaratibu, Waziri wa Nishati Mh. January Makamba, amemteua Bi.Zawadia Nanyaro kuwa mmoja wa wajumbe wa Bodi ya shirika hilo.
KUHUSU DCB
Benki ya Biashara ya DCB imekuwa ikipiga hatua na kukuwa kila mwaka, ambapo hivi karibuni ilibadilisha muonekano wake kutoka ule wa zamani.
Benki iliweza kuboresha leseni yake kutoka kuwa benki ya Mkoa na kuwa Benki kamili ya biashara (DCB COMMERCIAL BANK) mwaka 2012.
DCB ni benki ya kwanza kuorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es salaam.
Benki imeweza kulipa gawio kwa wanahisa wake kwa kipindi cha miaka 13 toka kuanzishwa kwake.
Fursa ya utoaji huduma na bidhaa zinazokidhi viwango vya ushindani, Huduma za kidigitali kama huduma za simu ya mkononi (DCB PESA), huduma za internet banking pamoja na Visa, huduma za malipo ya Mastercard QR, Malipo ya kielectroniki ya GePG, Mawakala Zaidi ya 1000 na ATM zinazotumia huduma za Umoja switch ambazo zipo zaidi ya 300 nchi nzima zimeweza kufungua fursa kwa watanzania wengi Zaidi
Mizania inayokaribia billioni 200
Mikopo mbalimbali ikiwemo Mikopo ya vikundi, Mikopo ya mshahara, Mikopo ya biashara, mikopo ya makampuni na Mikopo ya ada inayosaidia kuwanyanyua watanzania kiuchumi.
Kwa Kuhakikisha DCB inakuwa changuo la kwanza kwa wateja wetu, tunahakikisha wanaendelea kufurahia huduma na bidhaa zetu. Tunasisitiza kuwa benki itaendelea kutekeleza dira na dhima ya kuanzishwa kwake kwa kutumia fursa zilizopo ili kutoa huduma za kibenki kwa Wananchi na kuboresha maisha ya kila mtanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment