Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Monday, 16 August 2021
ZANTEL YABORESHA MAWASILIANO ZANZIBAR
Zanzibar - Katika jitihada za kuboresha huduma za mawasiliano visiwani Zanzibar, Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, imezindua minara nane ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali yaliyokuwa na mtandao hafifu ili kuhakikisha wateja wanapata huduma bora.
Minara hiyo iliyopo katika vijiji vya Seacliff, Kisiwa Uzi, Bumbwini Mafufu, Kisiwani, Chambani, Makangale, Maziwa N’gombe na Jongowe imezinduliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi - Zanzibar, Rahma Kassim Ali.
Akizunguza wakati wa hafla ya uzinduzi, Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa alisema lengo ni kuhakikisha Zanzibar yote inapata huduma bora na za uhakika za mawasiliano pamoja na mtandao wa intaneti.
“Zantel tumeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha huduma za mawasiliano hapa Visiwani Zanzibar.Leo tuna furaha kukamilisha minara hi inane mipya ambayo itasaidia katika kuongeza ufanisi wa huduma kwa wateja wetu,” alisema.
Aliongeza “Mbali na kusogeza huduma za kupiga simu kwa watu, dhamira ya Zantel kwa sasa ni kuendeleza matumizi ya intaneti na mfumo wa kidijitali katika masoko yetu. Tunaendelea kuboresha mtandao wetu wa intaneti kutoka kasi ya 2G na 3G na kuweka mtandao wa 4G katika baadhi ya maeneo,” aliongeza.
Pia, aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupitia Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji pamoja Wakala wa Miundombinu ya Tehama (ZICTIA) kwa kushirikiana kwa karibu na kampuni ya Zantel ambapo mpaka sasa zaidi ya asilimia 86 ya Zanzibar imeunganishwa na mtandao.
Kupitia ushirikiano na ZICTIA, Zantel imefanikisha kuunganisha zaidi ya minara 33 kwenye mkonga wa Mawasiliano (Fibre) kwa zaidi ya kilomita 28 ambayo imesaidia kuongeza ufanisi wa huduma.
Akizindua minara hiyo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi - Zanzibar, Rahma Kassim Ali aliipongeza Zantel kwa uwekezaji mkubwa ambao imeufanya katika kuboresha miundombinu ya mawasiliano kote Unguja na Pemba.
“Kampuni ya Zantel imekuwa karibu sana na serikali katika kutatua changamoto za mawasiliano zinazowakabili wanachi wetu wa Zanzibar, ninawapongeza sana kwa hili,” alisema.
Aliongeza “Mawasiliano ni muhimu sana katika upatikanaji wa taarifa sahihi zinazofika kwa wakati sahihi ili kufanya maamuzi ya kimaendeleo. Ndiyo maana serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za Kujenga miundombinu madhubuti ya TEHAMA kama vile Mkonga wa Mawasiliano wa Taifa na vituo vya kutunzia taarifa (data centre) ambayo imesaidia kukuza mawasiliano nchini na kuhakikisha usalama wa mawasiliano.”
Alisema kuwa, kuimarika kwa huduma za mawasilaino kutachangia kukuza uchumi wa Bluu kwa kuimarisha upatikanaji wa taarifa za masoko katika sekta hiyo.
Aidha, Zantel imechukua hatua kadhaa katika kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa intaneti kupitia kampeni yake kabambe ya PASUA ANGA KI ZANTEL 4G ili wateja waweze kuelewa umuhimu wa mtandao na kuweza kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment