Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 2 August 2021

VODACOM YAKAMILISHA KAMPENI YA 'TWENDE MJINI NA M-PESA'

Mshindi wa jumla kwenye kampeni ya 'Twende Mjini na M-Pesa', Neema Ikolo akionyesha plate number za gari alilokabidhiwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  • Yakabidhi gari aina ya Toyota cruise kwa Mwanamke
KAMPUNI ya Vodacom yakamilisha Kampeni yake ya "twende mjini na M-Pesa "kwa kuwakabidhi zawadi zao washindi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao, Mkuu wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani wa Kampuni ya Vodacom,  Brigta Stephen amesema tulitoa bajaji moja kila wiki kwa wiki 8 na leo inatoka gari aina ya Toyota Cruise.

"Unapokua na M-Pesa inarahisisha maisha kutokana na kulipia mahitaji mbalimbali kama Luku, kununua bando na vingine vingi hivyo utaona mtandao wetu ulivyokua na faida na leo tumekabidhi pikipiki 5 kwa washindi , bajaj moja pamoja na gari aina ya Toyota Cruise "

Stephen ametoa rai kwa watumiaji wa Vodacom kuendelea kutumia mtandao huo vizuri ili waweze kufaidika na zawadi mbalimbali zinazotolewa na Vodacom.

Hata hivyo amewataka waliopokea zawadi hizo kuwa mfano mzuri na kuutangaza vizuri mtandao huo.

Huku Mwakilishi wa Mkuu wa kitengo cha Mkakati kutoka M-Pesa, Nelusigwe Mwangota ameeleza jinsi gani kampeni hiyo ilikua na lengo la kuwashika mkono wa Tanzania na kuishi maisha ya kidigitali kutokana na kutumia Mpesa na kuwawezesha kufanya miamala kwa urahisi na kulipia bili mbalimbali.

"Tumeendelea kuwa wabunifu ambapo tumekua tukitatua matatizo mbalimbali tumebuni M-Pawa, M-Koba, Songesha huduma zote hizi ni kwa ajili ya kuwezesha kupata mkopo kwa haraka."

Pia amesema wanawake wamekua wakiachwa nyuma lakini katika kampeni hii haajaachwa mtu tumekuwa pamoja na ndio maana Mshindi wa gari ni Mwanamke.

Promosheni ambayo imechukua jumla ya wiki 8 katika Mikoa mbalimbali na leo imefika tamati kwa kuwakabidhi zawadi za washindi wa Mkoa wa Dar es salaam ameongeza Mwangota.

Kwa upande wake aliyeibuka Mshindi wa gari aina ya Toyota Cruise mpya 2021, Neema Ikolo ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuendesha kampeni hiyo ya 'Twende Mjini na M-Pesa' ambayo imetimiza ndoto za watu wengi ikiwemo yeye binafsi.

"Mara ya kwanza napigiwa simu sikuamini kabisa nilijua ni matapeli lakini baadae ni kapokea simu nikamsikia Salama Jabir aliongea ndipo nilipoamini nashukuru sana Vodacom kwa kampeni hiyo itakayoenda kubadilisha maisha ya wengi sana hususani watu wenye hali ya chini."

Hata hivyo Ikolo ameeleza sababu ambayo anahisi imemfanya kuibuka mshindi wa gari katika kampeni hiyo.

"Kiukweli Mahitaji yangu yote na manunuzi ya vitu nalipa kwa kutumia M-Pesa ndio sababu iliyochangia kushinda kwangu shindano hili.

No comments:

Post a Comment