Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mark Ocitti akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya uwekezaji kwa jamii wa kampuni hiyo uliyofanyika wajijini Dar es Salaam hivi karibuni. |
Kwa Tanzania miradi ya uwekezaji kwa jamii inatekelezwa na kampuni tanzu ya EABL, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL). Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, programu ya kilimo biashara inayowasaidia wakulima wazawa, unywaji wa kistarabu, programu za ujumuifu pamoja na utunzaji wa mazingira kupitia kupanda miti. Miradi hiyo inatekelezwa chini ya mpango wa kusaidia jamii unakwenda mpaka 2030.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti alielezea baadhi ya miradi inayotekelezwa na kampuni hiyo akianza na miradi ya kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama ambapo alisema SBL imeweza kuwafikishia huduma hiyo muhimu Watanzania milioni mbili ikilenga kurudisha kila tone inalotumia katika uzalishaji wa bidhaa zake. SBL imetekeleza miradi 21 ya maji hapa nchini tangu mwaka 2010.