Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa ndani wa benki hiyo, Douglas Bashobeza amesema wafanyakazi wameonyesha mwitikio wa kipekee na ili kuokoa maisha ya Watanzania wengi wenye uhitaji wa damu.
“Niwashukuru wafanyakazi wa benki ya Equity kwa kuonyesha moyo wa upendo na kujitolea damu hapa leo. Benki ya Equity tunaonyesha kwa vitendo kauli yetu isemayo “Tupo Pamoja” kwa kuyafikia makundi mablimbali ya jamii. Hii ni sehemu ya huduma kwa jamii ambayo benki yetu ya Equity inasikia fahari kujumuika na ninatoa wito kwa watanzania wenzetu kujitokeza kwa wingi kuja kuunga mkono,” amesema Bashobeza.
Kila tarehe 14 Juni nchi zote duniani huadhimisha siku ya kimataifa ya kuchangia damu ili kuwawezesha wote wenye kuwa na mahitaji hayo.
“Kila mtoaji damu anaweza kusaidia kuokoa maisha hadi ya watu watatu. Ishara hiyo ya upendo ni chanya sana hata katika afya zetu. Watu wenye kuwa na damu nyingi, wanaboresha pia afya yao katika kutoa zawadi hiyo na shukrani kwa vipimo maalum ambapo pia katika utoaji damu unawezekana kugundua pia ugonjwa mapema unaoanza katika mwili wako na kutibiwa mapema. Ni suala la kutengeneza uwezekano wa kutunza afya yetu na kuhisi zaidi uwajibikaji wa kuchagua mtindo wa maisha yaliyo bora” alisema mmoja wa waandaji wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment