Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday, 9 June 2021

RAIS SAMIA AMTEUA AFISA MTENDAJI MKUU WA BENKI YA NMB KUCHAKATA HAKI ZA WANAWAKE KIUCHUMI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Bi. Ruth Zaipuna akipongezwa baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa mmoja wa wanawake watakaoshiriki mchakato wa kujadili na kupatia ufumbuzi Haki za Wanawake Kiuchumi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Bi. Ruth Zaipuna akiwa miongoni mwa wanawake zaidi ya 10,000 walioshiriki katika mkutano wa Rais uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jiini Dodoma.
Afisa Mtendaji wa Benki ya NMB - Ruth Zaipuna akifurahia pamoja na wenzake mara baada ya kushiriki Mkutano wa Rais jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, kuwa mmoja wa wanawake watakaoshiriki mchakato wa kujadili na kupatia ufumbuzi Haki za Wanawake Kiuchumi.

Rais Samia ameyasema hayo jana, wakati akihutubia Mkutano wa Wanawake uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, ulioshirikisha takribani wanawake 10,000, wakiwemo wabunge wanawake, madiwani, wajasiriamali na Mama Lishe, waliowawakilisha wanawake wote nchini.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais Samia alieleza mikakati mbalimbali ya Serikali yake inayolenga kuleta Usawa wa Kijinsia, moja ya eneo ambalo yeye aliposhiriki Mkutano wa Afrika na Ufaransa kwa njia ya video, alilichagua baada ya kupewa heshima ya kuchagua eneo la Kumjenga Mwanamke wa Afrika.

"Wakati wa Mkutano wa Afrika na Ufaransa, uliofanyika kwa njia ya video, kwenye suala la Usawa wa Kijinsia, nilipewa heshima ya kuchagua eneo moja la Kumjenga Mwanamke ili tulisimamie na tuwe 'championi' wa eneo Hilo.

"Tanzania tumepewa heshima hiyo na Mimi nikachagua eneo la Haki za Kiuchumi kwa Mwanamke, kwa kutambua kuwa eneo hilo ni nguzo muhimu sana katika kuleta Usawa wa Kijinsia.

"Hivyo basi, naomba wadau tushirikiane katika hilo. Najua kati yetu hapa, nina vijana wazuri kwenye mabenki, wakiongozwa na ndugu yangu wa NMB (Afisa Mtendaji Mkuu, Ruth Zaipuna). Huyu ni mmoja kati ya Wanawake niliowachagua watakaoshiriki jambo hili, sambamba na wengine walio kwenye Sekta ya Uchumi," alisema Rais Samia.

Alibainisha kuwa, Zaipuna na wanawake wengine aliowachagua, jukumu lao kuu litakuwa ni kumsaidia Rais kufanya uchambuzi yakinifu na wa kina juu ya hali halisi ilivyo katika suala zima la Haki za Kiuchumi kwa Mwanamke ndani ya Tanzania na Afrika kwa ujumla wake.

Aliongeza kuwa, jopo hilo litapaswa kuangalia ni maeneo gani yana mapengo na maeneo gani Serikali za Afrika zingependa zisaidiwe na Ufaransa na mipango yao ni kwenda umbali gani, ambayo watayawasilisha kwa nchi hiyo ya Ulaya ili ione namna ya kuisaidia Afrika kufikia Usawa wa Kijinsia kupitia Haki za Kiuchumi kwa Mwanamke.

No comments:

Post a Comment