Kukwama kwa wajasiliamali katika sekta ya kilimo kushindwa kupata mikopo ya kifedha kutoka taasisi za kibenki imetajwa kuchangiwa na vikwazo vinavyotokana na changamoto ya ubora wa mazao yanayozalishwa na kupelekea kusababisha ukosefu wa masoko hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kizimba Business Model uliofanyika katika viwanja vya SUGECO Morogoro, Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Benki ya NMB - Isaac Masusu alisema kuwa mijadala ilikuwa mingi ya njia ipi itakuwa bora kwa benki kuweza kutoa mikopo ya muda mrefu katika sekta ya kilimo na sasa mfumo wa kilimo wa Kizimba Business Model itakuwa imefungua njia ya kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo.
Masusu alisema kuwa mfumo huo unawezesha vijana, akimama na wajasiliamali kuajiriwa katika sekta ya kilimo na mpango huo umejikita katika uwezeshaji upatikanaji wa ardhi ambao umekuwa kikwazo kikubwa kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuongeza thamani.
Masusu alisema kuwa moja ya kazi ya Benki ya NMB ni kushirikiana na SUGECO katika kufungua njia kwa wakulima ili kuwezesha kwa kushirikiana wadau wengine kufanya maeneo yanayosababisha mabenki kushindwa kutoa mikopo ya kilimo kwa makundi hayo kuwepo na suluhu.
Benki ya NMB kwa sasa itaanza kutoa mikopo ya muda mrefu ambayo wakulima watanufaika nayo kutokana na aina ya uwekezaji katika sekta ya kilimo, inayohitaji fedha nyingi na kwa muda mrefu, alisema Masusu.
Naye Waziri wa Kilimo - Profesa Adolf Mkenda alisema kuwa Sekta ya kilimo imekuwa ikiajili nguvu kazi nyingi hapa nchini lakini imekuwa haina tija- akitolea mafano zao la mchikichi nchini ya Indonesia na nchi nyingine duniani limekuwa na faida kubwa tofauti na Tanzania.
“Indonesia kwa hekta moja hupata tani 10 ya mafuta ya mawese wakati Tanzania hekta moja tumekuwa tukipata mafuta ya mawese tani 0.6, ni dhahiri kuwa lazima tuboreshw kilimo chetu ili kilete tija”alisema Profesa Mkenda.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro, Profesa Raphael Chibunda alisema kuwa chuo hicho ni wadau wakubwa wa Sekta ya Kilimo na kupitia SUGECO imefanya mabadiliko na mageuzi makubwa kwa wanafunzi kujifunza zaidi.
No comments:
Post a Comment