Washindi 12 wa droo ya mwezi wa pili ya NMB Mastabata Siyo Kikawaida, wamepatikana jana na kujizolea zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 28.8, hivyo kufanya zawadi zilizotolewa kufikia thamani TZS 87.6 kati ya zaidi ya Sh. Mil. 200 zinazoshindaniwa.
Promosheni ya Mastabata Siyo Kikawaida inayoendeshwa na Benki ya NMB, ni kampeni inayolenga kuhamasisha matumizi na manunuzi kwa Kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR, ilianza Novemba 24, 2020, ikitoa zawadi za Sh. 100,000 kwa washindi 40 kila wiki na washindi 12 wa Sh. Mil. 2.4 kila mwezi kila mmoja.
Akizungumza wakati wa droo hiyo ambayo ni ya pili kati ya tatu za mwezi, Mkuu wa Biashara ya Kadi wa NMB, Philbert Casmir, amesema katika droo saba zilizotangulia (sita za wiki na mbili za mwezi), zimewawezesha washindi wapatao 304 kujizolea zawadi za TZS. 87.6
Casmir amebainisha kuwa, NMB Mastabata imebakisha droo 3 kukamilisha miezi mitatu ya kampeni hiyo, ambayo zawadi kuu 'Grand Finale'itakuwa ni ziara ya utalii Zanzibar, Ngorongoro ama Serengeti, iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB, ambako washindi watakuwa huru kuchagua zawadi mbadala.
"Wito wetu kwa wateja wa NMB kuendelea kufanya matumizi na manunuzi mbalimbali kwa Kadi za NMB Mastercard na Mastercard QR, ili kujiongezea nafasi sio tu ya kushinda zawadi za wiki na mwezi, bali ziara hii ya kitalii katika moja kati ya maeneo hayo matatu," amesema Casmir.
Katika droo ya leo, iliyofanyika chini ya usimamizi wa Ofisa kutoka Bodi ya Michezo Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Albert, washindi 12 walikuwa huru kuchagua zawadi zilizogawanywa katika makundi matatu, kila moja likiwa na zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 2.4.
Katika kundi la kwanza kulikuwa na zawadi ya simu ya Samsung Galaxy Note20 yenye thamani ya Sh. Mil. 2.4, kundi la pili friji, water dispenser, Microwave na Samsung A21 kwa pamoja. Kundi la tatu ni runinga (flat screen inchi 40) iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, laptop na simu aina ya Samsung A21.
No comments:
Post a Comment