Mbali na kutoa fursa kwa wahitimu wasio na kazi na sifa zinazohitajika kuajiriwa moja kwa moja, uwekezaji huo umeiwezesha NMB kuzalisha wafanyakazi wenye ujuzi na weledi mkubwa katika maswala ya kifedha na kibenki.
Wahitimu wa program ya mafunzo ya uongozi ya Benki ya NMB katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni; Agnes Nyanzala, Norma Shindika, Mathew Mandara, Grace Shechombo and Witness Mosha. |
Akizungumza wakati wa mahafali ya wahitimu watano wa mwaka huu wa programu hiyo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB - Filbert Mponzi, alisema mchakato huo si muhimu tu kwa Benki hiyo na washiriki wake bali pia kwa tasnia ya fedha na nchi kwa ujumla.
Nyanzala alisema kuwa kwa sasa wameiva vya kutosha na wana ari kubwa katika kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi na kwamba wako tayari kwa mamapambano ya kunyanyua ustawi wa NMB kuanzia mwaka ujao wa 2021.
Programu ya mafunzo kazini ya NMB ilianzishwa mwaka 2009 na kila baada ya miaka miwili benki hiyo uwatuma wataalamu wake wa raslimali watu kwenda vyouni kutafuta wanafunzi wenye vipaji wapate mafunzo ya vitendo ndani ya benki.
Lengo lake kuu ni kuendeleza bomba ya talanta ya watu wenye ujuzi kwa maeneo ya msingi ya biashara ndani ya benki na kuunda fursa kwa wahitimu wasio na kazi na sifa zinazohitajika ili kuendeleza ustadi katika mazingira ya kibenki.
No comments:
Post a Comment