Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 21 September 2020

BENKI YA NCBA YAZINDUA MATAWI MAPYA MAWILI ARUSHA

Benki ya NCBA yalenga kusaidia kuimarisha huduma za Kifedha kwenye sekta ya Utalii Arusha

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Ltd, Margaret Karume (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa benki hiyo, Bw. Gift Shoko (wa pili kulia) wakiongoza matembezi ya uzinduzi wa matawi mawili mapya ya benki hiyo mkoani Arusha. Matawi hayo ni Clock Tower iliyopo Fire Road katika jengo la TFA, pamoja na tawi la Sokoine iliyopo barabara ya Sokoine, jengo la Central Plaza.
Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Benki ya NCBA wakishiriki katika matembezi ya uzinduzi wa matawi mawili mapya ya benki hiyo mkoani Arusha. Matawi hayo ni Clock Tower iliyopo Fire Road katika jengo la TFA, pamoja na tawi la Sokoine iliyopo barabara ya Sokoine, jengo la Central Plaza.
Meneja wa tawi la benki ya NCBA lililopo mtaa wa Sokoine jijini Arusha, Francis Pondo (kulia) akimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw Richard Kwitega (kushoto) katika tawi hilo katika tukio la uzinduzi wa tawi hilo lililoendana na matembezi mafupi. Pamoja naye ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa NCBA Bank Tanzania Ltd, Margaret Karume (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa benki hiyo, Bw. Gift Shoko (wa tatu kulia).
Wafanyakazi na wakaazi wa jiji la Arusha wakishiriki katika matembezi ya kuikaribisha benki ya NCBA mkoani Arusha ambapo benki hiyo imezindua matawi mawili mapya mkoani hapo. Matawi hayo ni Clock Tower iliyopo Fire Road katika jengo la TFA, pamoja na tawi la Sokoine iliyopo barabara ya Sokoine, jengo la Central Plaza. Matembezi hayo yalishereheshwa na bendi ya Polisi.




Arusha - Benki ya NCBA Tanzania Limited (NCBA) ilifanya uzinduzi wa kihistoria wa matawi yao mawili mapya jijini Arusha jumamosi ya tarehe 19 Septemba 2020. Matawi haya mawili mapya ni Tawi la Clock Tower lililopo Fire Road, Jengo la TFA na Tawi la Sokoine lililopo barabara ya Sokoine, Central Plaza ghorofa ya chini.

Hafla hiyo ya uzinduzi ni miongoni mwa matukio yanayoendelea kusherekea ujio wa, Benki ya NCBA, ambayo ni muunganiko wa hiari kati ya NIC (T) Limited na CBA Bank (T) Limited ambapo huduma rasmi za taasisi hii mpya ya Kifedha zilianza Julai 8, 2020 baada ya idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Mgeni rasmi wa hafla hio alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye aliisifu Benki ya NCBA kwa juhudi zao za kuchochea uchumi wa Tanzania. Alisema, ‘Benki ya NCBA imewasili nchini kwa wakati sahihi kabisa, mara tu baada ya Tanzania kujumuishwa kama nchi yenye kipato cha kati huku kukiwa na kiu cha kichocheo kipya kitakachoimarisha nafasi yetu mpya kiuchumi’.

Waziri alielezea kwa kina sehemu muhimu zinazohitaji msaada wa Kifedha mkoani Arusha baada ya athari za ugonjwa wa COVID19. Alinukuliwa, ‘…changamoto zozote zinazoikumba sekta ya utalii zina athari kubwa ambayo moja kwa moja inaathiri sekta nyingine zote za uchumi wa mkoa huu. Hapa Arusha, utalii ukipiga chafya, mji mzima unapata mafua. Na utalii wa Arusha ukipata mafua, basi hali ya utalii nchini kote huambukizwa homa. Hii ni kwa sababu asilimia kubwa ya watalii wanaokuja nchini hutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana katika ukanda huu wa kaskazini.


Hata hivyo hivi karibuni tumeanza kuona shughuli za Utalii zikirejea na kuonesha matumaini makubwa ya sekta kuwa kama awali, kurejea kwa shughuli za utalii zitasaidia kuchochea shughuli zingine za kiuchumi. Hivyo nitumie nafasi hii kuhamasisha Banki yenu kusaidia ustawi wa shughuli za Utalii nchini kwa kutoa mikopo ya riba kidogo na kuhairisha ulipaji wa mikopo kwa watoa huduma wa shughuli za Utalii nchini ili kuchochea ukuaji wa sekta hii muhimu kwa uchumi’.

Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Mhe Richard Kwitega alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Idd Hassan Kimanta alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla hiyo. Aliikaribisha Benki ya NCBA mkoani Arusha na kufafanua maeneo muhimu ya kiuchumi wa mkoa huo. Alisema, ‘Mkoa wa Arusha una fursa kubwa za uwekezaji katika kilimo na biashara husika ambapo mazao ya chakula, kilimo cha bustani na ufugaji kwa ajili ya usalama wa chakula, matumizi ya viwandani na kuuza nje hufanywa. Pia kuna fursa ya kukuza ufanisi katika kilimo cha ufugaji wa samaki’.

Alitoa wito kwa Benki ya NCBA kwa kusema, ‘Ni matumaini yangu, Benki ya NCBA imejizatiti kuwainua wakulima katika wigo mzima wa mnyororo wa thamani wa kilimo, kutoka mashambani hadi viwandani. Hii itabadilisha sekta hii muhimu ya uchumi kwa mkoa ili faida zinazopatikana ziifikie jamii na watu binafsi. Bila shaka, hauwezi kuutaja mkoa wa Arusha bila kuzungumzia utalii ambao unachangia zaidi ya 17% kwenye Pato la Taifa’.

Vilevile Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NCBA Bi Margaret Karume, aliwashukuru sana wenyeji wa mkoa huo na wageni waheshimiwa kwa kukubali mwaliko wao katika hafla hio na kuikaribisha Benki yao kwa dhati na kuahidi kuwa Benki itakuwa nao bega kwa bega katika safari ya kihistoria na ya pamoja ya mafanikio. Alisema Margaret,

‘Benki ya NCBA inaleta kwa pamoja ubora wa dunia mbili. Kuchanganya nguvu za taasisi mbili za awali zinaifanya benki ya NCBA kuwa benki kubwa, na yenye nguvu kifedha, yenye utaalam na uwezo mkubwa unaowaweka wateja wake mstari wa mbele katika kupata mafanikio’. Aliendelea kusema, ‘tutafikia malengo yetu kwa kutoa huduma na bidhaa mbali-mbali zita-kazowezesha wateja wetu wa mashirika na wateja binafsi kufanikiwa zaidi kwenye mipango yao. Hii, kwa upande mwingine, itasaidia kufikia matarajio ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Benki ya NCBA inathamini mahusiano na wateja wetu, na utoaji wa huduma bora kwa kiwango cha kimatiafa ndio kiini cha kila kitu tunachokifanya. Tunaamini kuwa uhusiano mzuri na wa kudumu unajengwa na mafanikio ya kila mmoja’.

Benki ya NCBA imezindua matawi 2 mkoani Arusha, yakiwa miongoni mwa matawi 12 mapya nchini baada ya kuzindua Makao ya Makuu ya ofisi na tawi mkoani Dar es Salaam mnamo tarehe 19 Agosti 2020. Benki ya NCBA inatazamia katika siku zijazo kuzindua matawi yake mapya ambayo tayari yameanza kutoa huduma katika mkoa wa Mwanza na visiwani Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:-
NCBA BANK TANZANIA LIMITED
Caroline Maajabu Mbaga
Mkuu; Masoko, Mawasiliano na Uraia
Barua Pepe: caroline.mbaga@ncbagroup.com
Simu: +255 (22) 2295000 / DL: +255 768 987008

Let’s GO FOR IT!

ABOUT NCBA BANK (T) LTD
NCBA Bank (T) Limited is a result of the merger of NIC Bank (T) Limited and CBA Bank (T) Limited. The merger follows through the successful acquisition of the majority of the assets and all of the liabilities of CBA by NIC. The Notice of Transfer of Assets and Liabilities was published in the Government Gazette on 17th January 2020 (as GN No.48) and in leading local newspapers. The Notice of Transfer of Assets and Liabilities was issued in line with section 4 of the Transfer of Businesses (Protection of Creditors) Act, Cap 327 R.E 2002.

The issuance of a banking license by The Bank of Tanzania paves the way for the two organizations to start operating as NCBA Bank (T) Ltd officially.

The merger creates one of the largest financial services groups in the region, a bank with the financial strength, expertise, and regional reach to support Tanzania and the regions’ economic growth aspirations. The group is strongly placed to play a bigger and more significant role in the banking sector and economies of Tanzania, the region and beyond.

It brings together the best in class retail and corporate banks with strong potential for growth in all aspects of banking and wealth management.

The merged entity will be a Universal Bank suitable and relevant for a wide demographic of customers, providing a full range of financial products and services for corporate, institutional, SME and consumer banking customers, who will benefit from strong relationship management and customer service excellence.

A proudly African Bank operating as an international bank with global standards, NCBA Bank is;

• One of the largest banks by customer numbers in Africa with a complementary base of over 40 million customers across Africa and the region, a strong digital proposition and a robust corporate and asset finance offering. NCBA Bank currently has 12 branches in Tanzania in Dar es Salaam, Arusha, Mwanza and Zanzibar.

• Amongst the largest financial institutions in the East Africa region and the 3rd largest Bank in Kenya with a total asset base over KES 444 Billion (Tsh 9,324bn) and Shareholders’ Equity of KES 65 Billion (Tsh 1,365).

No comments:

Post a Comment