Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 21 September 2020

BENKI YA NCBA YAANDAA MASHINDANO YA GOLF JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za Kidigitali wa Benki ya NCBA, Bw Gift Shoko akishiriki katika mashindano ya NCBA Golf Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Arusha kama sehemu ya uzinduzi wa matawi mapya ya benki hiyo katika mkoa wa Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizindua rasmi mashindano ya NCBA Golf Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Arusha. Mashindano hayo yaliyokuwa sehemu ya uzinduzi wa matawi mapya ya benki ya NCBA jijini Arusha yalilenga kukuza sekta ya utalii na ukuaji wa biashara.
Wadau mbali mbali wa michezo na biashara wakijadiliana jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) wakati wa uzinduzi wa mashindano ya NCBA Golf Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana Arusha. Mashindano hayo yaliyokuwa sehemu ya uzinduzi wa matawi mapya ya benki ya NCBA jijini Arusha yalilenga kukuza sekta ya utalii na ukuaji wa biashara nchini.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa na wadau mbali mbali wa michezo na biashara walioshiriki katika mashindano ya NCBA Golf Tournament yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana Arusha. Benki ya NCBA imefungua matawi mawili mapya katika barabara ya Sokoine na Ohio - Fire Road mkoani Arusha.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipokea maelezo jinsi ya kucheza mchezo wa golf kutoka kwa mojawapo ya wadau wa mchezo huo na mjumbe wa klabu ya Gymkhana, Bw Ruta Chubiriwa. Waziri Kigwangalla alikuwa anazindua mashindano ya NCBA Golf tournament yaliyolenga kukuza sekta ya utalii na ukuaji wa biashara.

No comments:

Post a Comment