Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 6 March 2020

VODACOM TANZANIA YADHAMINI WIKI YA UBUNIFU 2020

Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania PLC, Bi. Rosalynn Mworia (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu 2020 (Innovation Week 2020) jana jijini Dar Es Salaam. Katika wiki hiyo ya Ubunifu ambayo kauli mbiu yake ni "Buni kwa Tija" Kampuni ya Vodacom inatarajia kuonyesha bunifu zake mbalimbali katika sekta ya Kilimo, Elimu, Fedha na Afya. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo UK AID, Natalie Smith na Mkurugenzi Mkazi wa HDIF, Joseph Evarist.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu (wapili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu 2020 (Innovation Week 2020) jana jijini Dar Es Salaam. Katika wiki hiyo ya ubunifu ambayo kauli mbiu yake ni "Buni kwa Tija" Kampuni ya Vodacom ni mdhamini mkuu wa maadhimisho hayo. Wengine toka kushoto ni Naibu Mwakilishi Mkazi UNDP, Sergio Valdini, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania PLC, Bi. Rosalynn Mworia, na Naibu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo UK AID, Natalie Smith.
Mkurugenzi Mkazi wa HDIF, Joseph Evarist akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu 2020 (Innovation week 2020) jana jijini Dar Es Salaam. HDIF na COSTECH ndio waandaaji wa Wiki ya Ubunifu 2020 (Innovation Week).
Naibu Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo UK AID, Natalie Smith akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu 2020 (Innovation Week 2020) jana jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment