Zawadi hizo zinahusisha bidhaa za kisasa na za kibunifu zikiwemo simu janja aina ya Samsung A30, A70, A50, home internet routers pamoja na Playstation aina ya Sony.Bei ya chini ya kuanzia ni Sh1,000/-.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Mtaalamu wa Huduma za Kidigitali wa Tigo, Ikunda Ngowi alisema promosheni hiyo imelenga kutoa shukrani zao kwa wateja kwa kuendelea kutumia mtandao wa Tigo na pia kuwapa wateja jukwaa litakalowawezesha kununua bidhaa kwa bei pungufu.
“Tunafurahi kuzindua rasmi promosheni hii na tunaamini kuwa itawapa nafasi wateja wa Tigo kupata bidhaa za kidigitali kwa gharama nafuu, huduma hii ni ya haki na inampa kila mteja nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kulingana na thamani yake,” alisema.
Tigo inatambulika kama kampuni inayoongoza sokoni kwa kuchochea ukuaji wa huduma za kidigitali kwa kupitia teknolojia za kibunifu zinazotoa suluhisho katika maisha ya watanzania.Promosheni ya Toa bei ushinde (Bid-2-Win) itawapatia wateja bidhaa kwa bei pungufu ili kuwapa nafasi ya kufurahia maisha kwenye ulimwengu wa kidigitali.
“Kama kampuni ya kidigitali, tunatambua mahitaji ya wateja wetu na siku zote tupo mstari wa mbele kuleta suluhisho zenye kuboresha namna watu wanavyotumia huduma za mawasiliano. Huduma hii inamruhusu mteja kutoa bei ya bidhaa husika na kumpa nafasi ya kushinda.Tunaamini kupitia promosheni hii tutafungua njia kwa watanzania wengi kumiliki teknolojia za kidigitali,” alisema Kimsingi, Toa bei na Ushinde ni huduma ambayo itampa nafasi mteja kushinda bidhaa aipendayo kila wiki.Huduma hiyo pia itapungumza makali ya bei za bidhaa na kuwapa nafasi wateja kumiliki bidhaa wazipendazo kwa gharama nafuu.
Ngowi aliwahimiza wateja kushiriki kwa wingi katika promosheni hiyo kwani kadiri unavyoshiriki ndivyo unajiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.
Ili kushiriki mteja wa Tigo anaweza kutuma Ujumbe mfupi (SMS) wenye neno BID kwenda 15371.Kila meseji itatozwa kiasi cha Sh50 na washindi watapatikana kila wiki.
Kuhusu Tigo
Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo ni kampuni inayoongoza katika utoaji wa huduma kidigitali hapa nchini.Tigo ilianza kutoa huduma zake mwaka 1995 ikiwa na huduma mbalimbali za sauti, jumbe (SMS), intaneti yenye spidi pamoja na huduma za kifedha.
Tigo imekuwa mstari wa mbele kuleta mapinduzi ya kidigitali ikiwamo kuanzisha huduma ya Simu janja (Smartphone) ya Kiswahili, Facebook ya bure, App ya Tigo Pesa na zaidi kuwa kampuni ya Kwanza kutoa huduma ya kutuma na kupokea pesa katika nchi za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment