Meza Kuu ikifurahia jambo mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma za Fedha uliofanyika jijini Dar Es Salaam jana. |
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha iliyobeba kauli mbiu ya "Takwimu ni Mafuta Mapya" na kuwataka watoa huduma kuitumia kauli hiyo ipasavyo na kwa manufaa yenye kuleta tija.
Prof. Luoga amesema kuwa ufunguzi huo wa daftari la nguvu ya kitakwimu za kijiografia kwenye ukuaji wa soko uliowakutanisha wasimamizi wa sekta ya fedha wa watoa huduma za kifedha (FSR) ni endelevu huku mlengo mkuu ukiwa ni kuonesha mahali ambapo vituo vinavyotoa huduma za kifedha nchini.
Amesema kuwa daftari hilo la kwanza la aina hiyo litakuwa daftari la kwanza katika nchi za Afrika chini ya jangwa la Sahara na litajiendesha lenyewe katika mchakato wa kukusanya takwimu na kutoa upatikanaji wa taarifa kwa kidigitali moja kwa moja na daftari hilo litatumika kama mfumo wa taifa wa kufuatilia ukuaji na mgawanyo wa vituo vinavyotoa huduma za kifedha na kuwataarifu wadau wakuu wa mpango wa taifa na huduma jumuishi za kifedha kwa mwaka 2018/2022 na umma kwa ujumla.
Vilevile amesema kuwa Benki kuu ya Tanzania itatuma timu ya wakusanya taarifa nchi nzima ili kusajili vituo vinavyotoa huduma za kifedha na hiyo itajumuisha matawi ya benki, mashine za kutoa na kuweka fedha, wakala wa benki na wafanyabiashara na hiyo ni pamoja na wakala wa huduma za pesa kwa simu ya mkononi, SACCOs na benki ndogo za wafanyabiashara, taasisi, madalali wa bima na washauri walioteuliwa.
Imeelezwa kuwa usajili huo itafanyika kupitia programu ya simu iitwayo FRS Collect ambayo inapatikana kwenye simu zote zenye mfumo wa Android ambayo imetengenezwa na benki kuu ya Tanzania na kila atakayesajili atapata kitambulisho Cha FSR, cheti Cheney uwezo wa kusomwa na binadamu na QR.
Wasimamizi wa mchakato huo unaongozwa na Benki kuu ya Tanzania (BOT,) kwa kushirikiana na Tune ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na Mamlaka ya masoko ya Mitaji na dhamana (CMSA).
No comments:
Post a Comment